Msaada: Vituo vya kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo mkoa wa Dar es Salaam

jichopevu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
406
Reaction score
248
Habari wakuu,

Nina ndugu ndio amewasili hivi jijini Dar hapa na yupo yupo tu. Sasa sipendi tu awepo awepo hapa nyumbani, nimeona nimtafutie kitu cha kufanya chenye manufaa nae. Hivyo nimeona mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo yatamfaa sana. Sasa kuna kituo kimoja kipo Banana kule (sikijui kilipo kwa hapo banana) nilisikia tu tangazo lake kwenye redio na nikachukua namba zao ila kwa bahati mbaya zile namba sijui nilizihifadhi wapi.

Hivyo kama kuna mdau anakijua hicho kituo au kama kuna sehemu yoyote unaijua ambayo haya mafunzo ya ujasiriamali kwa vitendo yanapatikana naomba unijulishe tafadhali. Jina la kituo, sehemu kilipo na mawasiliano yao kama unayo.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
 
Mkuu hakuna Mahali popote pale Duniani kuliko na kituo cha kufundisha watu Ujasirimali, Ujasiriamali ni hari so haufundishwi mkuu, bali kuna vituoa vya kufundisha maswala ya ufundi, na elimu ya biashara, ila si ujasiriamali
 
Mkuu hakuna Mahali popote pale Duniani kuliko na kituo cha kufundisha watu Ujasirimali, Ujasiriamali ni hari so haufundishwi mkuu, bali kuna vituoa vya kufundisha maswala ya ufundi, na elimu ya biashara, ila si ujasiriamali

Wewe unajua maana ya ujasiriamali ? Hizo ni fikra zako tu sio lazima wote tufikiri km wewe, unaweza potosha watu, inawezekana sana kufundisha ujasiriamali ! ! !
 
Awasiliane na CPM Business Consultants atapatiwa mafunzo ya ujasiriamali na ya utengenezaji wa bidhaa kama vile Sabuni, maji ya betri, ufugaji wa kuku, kilimo cha uyoga nk. Kwa mawasiliano zaidi nipigie simu 0784394701
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…