Msaada wa Aliexpress

Msaada wa Aliexpress

Grand Canyon

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2020
Posts
545
Reaction score
1,191
Niliagiza kifaa fulani huko Aliexpress 10/10/2020. Niliambiwa nitarajie kupata kifaa hicho kati ya Novemba 2-Desemba 2. Mpaka sasa naona kimya.

Uliwahi kuwa katika hali hii?

Ulifanyaje?
ALIEXPRESS.jpg
 
Kawaida unaweza hata kusahau kama uliagiza ndo kikafika ndo maana mimi nikitaka kuagiza kitu cha fasta nampigia mtu aliyeko china aninunulie anitumie moja kwa moja.

Hawa mwaka jana kuna mtu nilimwagizia nguo zikachelewa akaanza nisumbua sana ikabidi niingie kariakoo nikazisaka nikanunua, after 2 weeks ndo napigiwa sim zimefika, hata kuzifuata sikwenda maana nilikua nshavurugwa.
 
subiri kitafika tu ila siku nyingine tumia makapuni yanayosafirisha mizigo itakuwa haraka zaidi, maana kwa nch zetu naona bado mifumo haijakaa vizuri pia ukitumia kwa ndege unafika haraka zaidi'

Ila tumia makampuni yanayosafirisha kwa uhakika zaidi
 
ila tumia makampuni yanayosafirisha kwa uhakika zaidi

Makampuni gani hayo?
 
Kawaida unaweza hata kusahau kama uliagiza ndo kikafika ndo maana mimi nikitaka kuagiza kitu cha fasta nampigia mtu aliyeko china aninunulie anitumie moja kwa moja.

Hawa mwaka jana kuna mtu nilimwagizia nguo zikachelewa akaanza nisumbua sana ikabidi niingie kariakoo nikazisaka nikanunua, after 2 weeks ndo napigiwa sim zimefika, hata kuzifuata sikwenda maana nilikua nshavurugwa.
Imefika baada ya miezi 4! Nilishajikatia tamaa
 
Update: Siku hizi aliexpress wako vizuri, mzigo ukifika nchini wanakutumia email kwamba parcel yako sasa iko nchini. Basi unasubiri upigiwe simu na posta.
 
Mkuu hivi kuna haja ya kuwa na sanduku la posta?
 
subiri kitafika tu ila siku nyingine tumia makapuni yanayosafirisha mizigo itakuwa haraka zaidi, maana kwa nch zetu naona bado mifumo haijakaa vizuri pia ukitumia kwa ndege unafika haraka zaidi'

Ila tumia makampuni yanayosafirisha kwa uhakika zaidi
Yataje mkuu hayo makampuni
 
Mkuu hivi kuna haja ya kuwa na sanduku la posta?
Huitaji sanduku la Posta. Unachohitaji tu ni namba ya simu.Ili mzigo ukifika posta unapigiwa simu, Mr Johnman kuna parcel yake hapa posta njoo na kitambulisho cha nida au unaweza kumtuma mtu lakini aje na picha yako na nida yako. (Kama kuna gharama fulani utaambiwa njoo na Tsh 2,350/=)
 
Shukrani sana mkuu nimekupata vyema
 
m

mkuu sasa hapo kwenye Po Box unajaza nini kama huna sanduku la posta, msaada please.

2389078_Screenshot_20200504-201857.png
 
je hapo hizo details zingine ziko sawa...!?,
na kwa uzoefu wako mkuu mzigo mara nyingi huchukua muda gani kukufikia...!?,
samahani kwa maswali mkuu lakini.
Unajaza Majina yako, namba ya simu na mahali utakapokuwa unapokelea mzigo wako.
Niliagiza bidhaa ya Kwanza ikafika baada ya miezi 4, bidhaa ya pili ikafika baada ya siku 17, bidhaa ya tatu ikafika baada ya siku 35, bidhaa ya nne ulifika baada ya siku 20, nk nk. Kwa uzoefu wangu bidhaa za "free shipping" zinachelewa Sana. Niliagiza mizigo miwili kwa wakati mmoja ,nilioulipia nauli ulifika siku ya 35,ule wa free shipping sasa ni siku 50 haujafika.
 
Inaonekana una eperience ya kutosha naomba unidm namba yako ya whatapp mkuu
 
Back
Top Bottom