msaada wa bajeti please!

msaada wa bajeti please!

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
niko katavi nimeajiriwa kwenye kampuni fulani,mshahara kwa mwezi sh 300000 tatizo nashindwa kupanga bajeti hata hivyo nina mke na mtoto na nimepanga vyumba 2 vyote kwa sh 50000,nisaidieni jamani!
 
Pole sana Kiongozi!

Upangaji wa Bajeti kutegemea na Mshahara ni tatizo kubwa sana kwa Watanzania wengi walio katika Ajira. Hauko peke yako. Amini, usiamini, kuwa Waajiriwa wanapata Mishahara ya 5,000,000/= kwa mwezi, lakini linapokuja suala la kupanga bajeti ya Mshahara wake linakuwa tatizo kubwa kiasi cha kuishi katika mazingira magumu kuzidi hata yako mwenye Mshahara wa Sh. 300,000/=! Lakini kwa upanda mwingine, kuwa Watu ambao kipato chao kwa mwezi ni robo ya Mshahara wako kwa mwezi, wana maisha mazuri, yenye furaha na amani!

Mimi sio Mtaalamu wa mambo hayo. Mimi ni mmoja wa Wahanga wa Tatizo hili la kushindwa kupanga Bajeti za Mishahara yao. Niko katika Mkakati wa kupunguza na hatimaye kutokomeza kabisa Tatizo hilo. Kwa misingi hiyo, ninapenda nikushirikishe Tiba ninayodhani inaweza kunisaidia mimi na wewe, nikichukulia Mshahara wako kama mfano:

Hitaji/Tumizi Asilimia Kiasi

01. Chakula - 30% - 90,000/=

02. Mavazi - 05% - 15,000/=

03. Pango - 17% - 50,000/=

04. Akiba - 12% - 35,000/=

05. Matibabu - 10% - 30,000/=

06. Mradi - 18% - 55,000/=

07. Sadaka - 03% - 10,000/=

08. Mengineyo - 05% - 15,000/=

Jumla 100% 300,000/=

Kwa sasa ninaomba niishie hapa. Nitarejea baadaye na “utetezi” wa mchanganuo wangu, tukitarajia Wadau wengine watakuja na michango na Elimu zaidi! Baadaye kidogo!
 
Asante sana mahina veterani nitajaribu hiyo nione

Nimerejea Mkuu, kama nilivyoahidi. Usiwe na haraka ya kunifukuza kabla sijatoa "utetezi" kwenye Mchanganuo wangu!

Kabla sijaenda mbali, naomba nikukumbushe na nikupe angalizo - Mimi siyo Mtaalamu, ni Muhanga kama wewe! Haya, tuanze:

1. Chakula = 30% = Sh. 90,000/=:
Sijawahi binafsi kufika Katavi. Lakini kutokana na kusoma maadniko kadha wa kadha ninaamini Katavi ni moja ya sehemu chache hapa Nchini zenye neema kwa upande wa Chakula. Ninachelea kuweka hata hiyo Bajeti kwa kuamini Chakula huko Katavi ni nafuu. Hata hivyo, Familia yako bado ni ndogo. Jitahidi, muhimu umshirikishe na Shemeji katika baadhi ya haya masuala, kununua Chakula kwa wingi hasa kisichoharibika haraka. Mfano: Mchele nunua Kilo 20, Unga (wa mahindi/mtama na mhogo) kilo 10; Mafuta ya kula Lita 20; Sukari Kilo 10; Dawa ya Mboga (huko kwenu mnaita Chumvi) Kilo 2; Dagaa (au Samaki wakavu) debe 1; Sabuni za miche miche 20, sabuni ya unga kilo 10, n.k., n.k., Kaa Kikao na Shemeji, atakuwa anayajua haya zaidi ya mimi na wewe. Nia hapa ni kukupa picha kuwa uachane na kununua chakula kwa rejareja, kwanza ni gharama halafu ni kujitafutia "msongo wa mawazo". Shauriana na Shem, jinyimeni, nunueni Chakula na mahitaji ya muhimu mwezi mmoja, na kila mwisho wa miezi inayofuatia, Shem apige hesabu ya "stock" iliyopo na mrudishie (restock).
Kama nafasi inaruhusu hapo unapoishi, lima hata tuta moja la Mchicha na tuta moja la Chinese kwa ajili ya mbogamboga ya matumizi yenu. Kumwagilia na kutunza matuta mawili ya miche kadhaa ya mbogamboga ni kazi rahisi, unaweza ifanya hata wakati unapiga mswaki kabla ya kwenda kazini. Ziada, uza ili upate pesa kidogo kwa matumizi madogomadogo ya nyumbani!
2. Mavazi = 05% = Sh. 15,000/=:
Samahani kwa hili sitakuweka wewe. Wewe ni Mwanamume bwana, Jeans pair 3 za mitumba, mashati kadhaa ya mitumba, raba za mitumba, nguo za ndani kadhaa, n.k. zinakutosha kabisa kwa Mwaka mzima! Utapendeza ukishapata. Kubaliana na Shem kwanza kabla hujaamua kukomaa kihivyo!
Ninaongelea Mke wako na Mwanao. Ni kiasi kidogo lakini kwa hali ilivyo, jaribu kuwapendezesha kadri ya hali. Sh. 15,000/= haitoshi kupeleka Wife Saloon kila wiki. Ukiongea naye, tajua namna ya kupendeza ndani ya bajeti. Mpendezeshe Mkeo – inakuepushia michepuko!
Mahitaji ya Mtoto wenu vile vile yazingatie hali halisi. Sijui Mtoto wenu ana umri gani, kama ana miaka 2+, basi pigisha vimitumba!
3. Kodi = 50% = 50,000/=:
Hili sina mjadala mkubwa. Ninachoshauri, angalia kama unapoishi panawapa nafasi ya kufanya na mambo ya ziada kama kulima angalau matuta 2 ya mbogamboga kama nilivyosema hapo juu na kuendesha ka-Mradi hata kadogo kama nitakavyoeleza hapa chini kwenye Na. 6. Kama hapakupi fursa hizo, basi tafuta kwingine. Haijalishi kama kuna Umeme na Maji au la. Hayo yatakuja baadaye. Cha msingi iwe sehemu yenye usalama!
4. Akiba = 12% = 35,000/=:
AKIBA! AKIBA! Sina hakika na Takwimu zangu, lakini kwa uzoefu ninaamini ukichukua Waajiriwa 20 hapa Nchini, utakuta pengine 03 tu wanajiwekea Akiba! Kwa kawaida tunatakiwa tuifanye Akiba kama Deni ambalo ni lazima lilipwe! Wengi tunakuwa katika mzunguko wa matatizo kwa kuwa hatuna hurka ya kujiwekea Akiba! Kama Mtu ukichukulia Akiba kama Deni ambalo lazima lilipwe kila mwisho wa Mwezi, basi baada ya muda mfupi utakuwa na Akiba kubwa unayoweza kukuwezesha kufanya makubwa.
Kwa sababu ya changamoto mbalimbali za maisha kwenye hali kama yangu na yako, nisingeshauri uweke Akiba Benki. Hii ni kwa sababu ya urahisi wa kuitumia hata kwa matumizi yasiyo ya lazima kwa sababu ya ATM! Tuwaache wenye Mishahara na Vipato vikubwa watunze Akiba zao huko. Mimi ninakushauri uweke Akiba yako kwa kujiunga na Vikundi vya Kuweka na Kukopa, wengine wanaviita VICOBA na wengine Vikundi vya Hisa, n.k.! Faida ya kuweka Akiba kwenye Vikundi hivyo ni lukuki. Hapa hapa kwenye JF search "VICOBA" au VSLA utapata nondo za kutosha. Ukikwama nenda pale Halmashauri ya Wilaya Idara ya Maendeleo ya Jamii, ulizia utapata maelezo ya kutosha. Mfumo wa VICOBA/Hisa umeenea kote Nchini. Ukikwama kabisa, tutaeleweshana tu!
Sasa tupige hesabu: Ukiweka Akiba kwenye Kikundi chako cha Kuweka na Kukopa ya Sh. 35,000/= X Miezi 12 = Sh. 420,000/= kwa Mwaka + Ziada/Faida itayozalishwa kutokana na Mikopo na Faini mtakayokuwa mnakopeshana kwenye Kikundi/Vikundi vyenu! Siyo mbaya. Ni mwanzo mzuri! "Mbuyu ulianza kama Mchicha"
5. Matibabu = 10% = 30,000/=:
Kama Kazini unayo Bima ya Afya, basi ni heri! Kama huna Bima ya Afya ya Kazini, basi ningekushauri uangalie uwezekano wa kujiunga na "Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya" kwa ajili ya Mkeo na Mwanao. Sina uzoefu sana na Mfuko huu unavyofanya kazi na ufanisi wake. NInachofahamu ukishajiunga, unachangia Sh. 10,000/= kwa mwezi. Ni muhimu kuwapa kinga Mkeo na Mwanao. Kama ni hivyo, Salio la Sh. 20,000/= weka kwenye Akiba kama nilivyoshauri hapo juu ili likitokea la kutokea iwe rahisi kuchota na kurekebisha hali. Kama halitokei lolote, basi itaendelea kuwa Akiba na kuzunguka!
Nimesisitiza Mkeo na Mwanao bila kukutaja. Wewe ukiugua maradhi madogomadogo, gonga glasi kadhaa za muarobaini tu! Wewe Mwanaume Bwana!
6. Mradi = 18% = Sh. 55,000/=
Kwa mtu mwingine kiasi hiki kunaweza kuonekana kidogo sana kufanya Mradi wa aina yoyote! Hilo sio kweli! Hiki ni kiasi kikubwa sana! Unaweza kuwa Milionea kwa kuanzia na Mtaji wa kiasi hiki. Nisingependa kusema mengi. Tuangalie mfano rahisi wa "Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji". Hapahapa JF kuna mamia ya Uzi zinazoongelea Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji. Hasa nilifurahishwa sana na Uzi mmoja ambao kwa bahati mbaya siukumbuki Jina na muda hauruhusu kuutafuta unaoongelea "Jinsi Kuku 1 anavyoweza kukuzalishia Sh. 1,000,000/=" Naamini, Katavi ni kama Miji midogomidogo iliyoenea hapa Nchini. Kuku wa Kienyeji nje ya Katavi, yaani Vijijini, ni kati ya Sh. 5,000/= - 8,000/=. Hivyo, kwa Sh. 55,000/= tayari na Jogoo 1, mitetea 6 na chenji inabaki kwa ajili ya matibabu yao ! Utajiri upo hapa hapa JF na kwenye Mitandao kadhaa ya Ujasiriamali. Shemeji ana ajira? Kama hana, basi usimamizi wa Mradi huo wa Kuku 7 ndiyo iwe ajira yake rasmi! Tafuta pango lenye kukupa unafuu wa kuendesha Miradi midogomidogo kama hii. Wewe na familia yako laleni kwenye Chumba kimoja, kuku walale kwenye chumba kingine. Asubuhi saa 12 wafungulieni, fanyeni usafi, mchana hiyo ni sebule! Ni kwa muda tu, hao kuku watakujengea Nyumba Self Contained baada ya muda mfupi!
NIsishauri ufanye Mradi kwa kuiga majirani, eti kwa kuwa "Mama Nanihii" wa Nyumba jirani ana Mradi wa kuuza Samaki na "anapatamo", basi na nyie mfanye! La hasha, kuweni wabunifu!
7. Sadaka = 03% = Sh. 10,000/=:
Sijui Wewe, Mkeo na Mwanao mnaabudu Imani gani. Lakini cha Msingi Ibada ni muhimu sana, haijalishi Dini, Dhehebu, n.k. Katika kile kidogo unachopata, zingatieni Ibada na Sadaka. Sina maana kiasi chote hicho kiende kwenye huko mnakoabudu. Kiasi, tuseme Sh. 5,000/=, toeni Sadaka kwenye Nyumba ya Ibada yenu, kinachobaki, tuseme Sh. 5,000/= tumieni kusaidia wenye shida mbalimbali kama Wagonjwa wasio na Msaada, Watoto wanaoishi katika mazingira magumu, Chakula kwa wenye Uhitaji zaidi yenu, n.k. Mungu Yupo, atawarejeshea mara elfu ya kile mnachotoa, iwe moja kwa moja kwa maana ya Mali ama kwa kuwajalia Afya njema!
8. Mengineyo = 05% = Sh. 15,000/=:
Hizi ni kwa ajili ya Shughuli za Kijamii, kusaidia Ndugu, Misiba ya Jirani, n.k. Kwenye hili hili, kila mwisho wa Mwezi kama kuna salio limebaki kwenye Mengineyo ya Mwezi unaoisha, sio vibaya mara moja moja ukaburudika na familia yako kwa kuitoa "out" hapo Katavi!
Nyongeza:
Nidhamu: Unatakiwa uwe na nidhamu ya hali ya juu ili "utokemo"! Kama ni starehe, waachie "walizo nazo". Utastarehe ukishapata! Kama unakamata "the Larger", basi kamata kwa malengo! Achana na "michepuko", haina manufaa. Mjali na mpende Mkeo na Mwanao!
Madeni: Epuka sana MADENI! Jaribu sana kuishi ndani ya uwezo wako! Fanya na timiza kinachowezekana, kisichowezekana achana nacho! Usikope kwa shinikizo la Mtu yeyote na usikope kwa mambo ya kupita!
Mkeo: Ninaogopa kulisema hili kwa kuwa sijui lolote kuhusu wewe na Mkeo, lakini ningeshauri umshirikishe Mkeo katika mipango ya nyie kujikwamua kimaisha!Kama ni Mke mwenye Busara, utafanikiwa ndani ya muda mfupi. Binadamu wote hatulingani, ni kweli. Kama ana mapungufu yake, basi tafuta namna ya kukabiliana nayo na kumchukulia kama BInadamu ambaye hakosi mapungufu. Isitoshe ni Mama wa Mwanao, hiyo ni Baraka ya pekee!

Kama nilivyosema hapo mwanzo, Mimi sio Mtaalamu. Ni Muhanga wa Tatizo la kushindwa Kupanga Bajeti na kufuata Bajeti ya Kila Mwezi. Kama kuna mapungufu katika niliyoandika, nisamehewe na nirekebishwe, itakuwa msaada kwangu!

Vinginevyo, tukutane Mwakani kupeana mrejesho! Ubarikiwe!
 
mkuu mahina veterani asante sana umemaliza kila kitu.Ngoja nianzekuyafanyia kazi nitakupa jibu
 
Nimefaidi sana na mimi kwa kweli, ila mkuu umejishusha mno, wewe ni mtumishi wa Bwana.
 
hapo kwenye sadaka nina wasiwasi napo mkuu ila kwingine uko poa,wakristo ni 10% zaka
 
huyu jamaa si mtu wa kawaida
kwa huo uchanganuzi, nasema jamaa anashughurika na maswala ya kiuchumi
nami nimefaidika sana , ahsante sana mkuu!
 
Jamaa ni muhanga wa kuhindwa kupanga bajeti (alipata shida sana kutokana na kushindwa kupanga bajeti) akajifunza, akapanga bajeti, akafanikiwa, hivi sasa anafundisha wengine maana hataki yawakute yaliyo mkuta ( HUU NI MOYO WA PEKEE)

Abarikiwe kwa elimu yake nzuri, he is a great thinker.
 
ndugu yangu kupanga bajeti inategemea na mshahara uupatao au ulionao
kitu cha kuzingatia ungeweza kupanga chumba cha 30,000 ili kupunguza gharama za kodi
kingine ni kununua vitu au mahitaji yote ya mwezi na kuyaweka ndani ili kujua mnatumiaje mfano chakula
kingine ni kujua matumizi yako yakoje kama wewe ni mtu wa kufuja mali usitegemee kuwa utaweza kupanga bajeti ila kama wewe ni mchumi mzuri utaweza kujilimbikia mali yako.

niko katavi nimeajiriwa kwenye kampuni fulani,mshahara kwa mwezi sh 300000 tatizo nashindwa kupanga bajeti hata hivyo nina mke na mtoto na nimepanga vyumba 2 vyote kwa sh 50000,nisaidieni jamani!
 
hapo kwenye sadaka nina wasiwasi napo mkuu ila kwingine uko poa,wakristo ni 10% zaka

Hebu tuwe wakweli jamani, hivi kwenye makanisa na misikiti tunapokwenda kwa ibada wangapi huwa wanatoa zaidi ya elfu kumi? asilimia ngapi wa waumini? Labda wale mafisadi wanaomwaga yale mamilioni lakini hawa wa mishahara 300,000 - 500,000/= kwa mwezi mimi sijaona! Na si kwamba hawataki kama maandiko yanavyosema lakini uchumi umebana bandugu!!
 
Nimejifunza mengi asante!
 
Back
Top Bottom