Ahsante sana mkuu pretaPoleni sana mkuu.......hapa JF utapata msaada wa kutosha....vuta subira......
pole sana mconsult dr.mbembati wa nh2
ahsante kwa ushauri mkuu, tupo dar mkuumbembati?! Labda ni tofauti na ninayemfahamu miye. Nendeni mnh mtahudumiwa. Mtapeleka hospital zingine wakamfanyia tapping aafu akafa. Hatuna hakika kama tatizo alilo nalo ni figo, moyo au ini. Nenda hospitali mtahudumiwa vizuri tu. Kwani uko wapi?
Wakuu tuna baba yetu anatatizo la kuvimba miguu na tumbo kujaa na moyo unamatatizo pia hali kabisa chakula, sasa tumepima hospital wamesema figo zinamatatizo pia tumboni kumejaa maji so inabidi tukanyonye hayo hospital, sasa kama kuna mtu anamfahamu dokta ambaye ni bingwa kwa mambo hayo na hospital anayopatikana naomba tusaidiane jamani
Nenda Muhimbili, ikiwezekana ingia Fast Track utapata huduma. Mtafute Dr O. Kisanga 0784 782948 au Dr Linda 0754 290499 naamini watamsaidia mzee. Poleni sana.
Ahsante sana mkuu, tumempeleka leo asubuhi muhimbili wamemuwekea dripu wamemlaza, ila me ni mgeni kidogo pale muhimbili fast track ndio sehemu gani hapo
Kuvimba miguu na tumbo kunaweza kusababishwa na matatizo ya figo, ini au moyo.
Kama ni tatizo la figo wasiliana na Dr Kisanga yupo Renal Unit pale Muhimbili. Nitaku-PM namba yake.
Ni kama private kiasi fulani ila inakuwa hapo Muhimbili. Pia wasiliana na hao ni Madaktari Bingwa ambao wataweza kukupa msaada.Poleni sana Mkuu.
Ahsante sana mkuu, ila ukinipm namba yake itakuwa vizuri zaidi mh.
Kuvimba miguu na tumbo kunaweza kusababishwa na matatizo ya figo, ini au moyo.
Kama ni tatizo la figo wasiliana na Dr Kisanga yupo Renal Unit pale Muhimbili. Nitaku-PM namba yake.
Siku zingine mnakuwaga watu wazuri sana. I am proud of you. Lakini siku zingine mmmmhhh sijui pepo gani huwa anawaingia!
Hivi mtu akiwa na mgonjwa anampigia simu daktari au anaenda naye hospitali?
Hii ya kumpigia simu daktari wa hospitali ya umma mbona imekaa kirushwa zaidi? au ndio utaratibu wetu Tanzania?
Nakushauri nenda na mgonjwa wako katika hospitali iliyo karibu na pale ulipo ili watathmini tatizo na wakiona hawawezi kumtibia mzee watakuandikia barua ya rufaa uende kwenye hispitali kubwa kama Muhimbili. Ukienda Muhimbili bila barua ya rufaa utasumbuka bila kumjua mtu.
Ukimpigia simu daktari moja kwa moja akakupa appointment kinachotokea ni kwamba manesi na watumishi wengine wa afya wanajua daktari umemuhonga kwa hiyo jiandae kuwa nao watataka hongo. Bila hongo watajisikia kama wanamfanyia kazi huyo daktari ajiingizie pesa za hongo peke yake. Hiyo ndio perception iliyopo.
Kama mfuko wako uko vizuri nakushauri umpleke mzee Tumaini Hospital ya Upanga.