Rutakyamilwa
JF-Expert Member
- Feb 27, 2009
- 1,871
- 1,237
Tafadhali naomba utaalamu wa wajuzi wa kilimo. Nina miembe ya kuunga ambayo inatoa maua. Mwaka jana ilitoa maua mengi lakini haikuweka maembe, maua yote yalipukutika. Mwaka huu ndiyo imetoa maua mengi sana. Wataalamu nisaidieni nifanyeje kuyanusuru maua hayo. Wenyeji wanamasema nyunyizia dawa, dawa hawaijui. Msaada please.