Wakuu, habari za wakati huu.
Nimekuja kwenu kuomba msaada wa dawa ya kupunguza kulala.
Nalala mapema sana, naweza kulala sa 1, sa 2 au hata sa 12 kama nimewahi kurudi nyumbani.
Nahitaji dawa angalau ya kuniweka macho angalau hadi sa 4 au sa 5 usiku. Hii ya kulala mapema inanikwaza sana. Nilipokua mdogo nilikua naweza kulala hata kuanzia sa 11 jioni. Na nilipokua mdogo zaidi naambiwa nikilala sa 11 jioni nitaamka kesho sa 5 au sa 4 asubuhi, watu walikua wanadhani nimekufa. Sasa hili naona linaniandama hadi sasa. Nilipokua nasoma shule ya bweni, naambiwa nikae prep hadi sa 4 ilinishida, sa 2 tu nishaenda kulala au nalala darasani.
Angawaje nawahi kuamka hata kama nikilala sa 10 ikifika sa 12 lazima niamke ila hii ya kuwahi kulala inaniboa sana.
Naweza kua mahala labda Bar ingawa sinywi pombe kwa ajili ya kubuy time ili nisiwahi kulala ila muda wote nahisi usingizi.
Naombeni msaada wa natural remedies au hata over the counter medications.
Ahsanteni sana.
MREJESHO.
Wakuu, nawashukuruni sana mlionishauri nitumie kahawa.
Kabla sijatoka ofisini sa moja hivi kasoro nikamuomba mama mhudumu wa ofisi aniandalie kikombe cha gawaha ila mara moja zaidi ya kipimo cha kawaida.
Toka nimefika nyumbani sa moja niko sebuleni natazama tv wala sijahisi aina yoyote ya usingizi kitu ambacho sio kawaida kabisa kwangu, ningekua nishalala sebuleni au kuhisi kwenda kulala muda mrefu sana.
Itabidi niweke kahawa kama kinywaji changu rasmi kunywa masaa kadhaa kabla ya kulala ili niwe nakua macho angalau hadi sa 4 au 5.
Ahsanteni sana. Karbuni tuangalie televisheni.
View attachment 1003839