Msaada wa dawa ya kupunguza usingizi

Msaada wa dawa ya kupunguza usingizi

Watu tunapishana...

Mimi natafuta dawa ya kulala...nina shida mbaya ya kutolala kabisa.
Nimehangaika na tiba nyingi tu ila bado!
Yaani nateseka sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu, habari za wakati huu.

Nimekuja kwenu kuomba msaada wa dawa ya kupunguza kulala.

Nalala mapema sana, naweza kulala sa 1, sa 2 au hata sa 12 kama nimewahi kurudi nyumbani.

Nahitaji dawa angalau ya kuniweka macho angalau hadi sa 4 au sa 5 usiku. Hii ya kulala mapema inanikwaza sana. Nilipokua mdogo nilikua naweza kulala hata kuanzia sa 11 jioni. Na nilipokua mdogo zaidi naambiwa nikilala sa 11 jioni nitaamka kesho sa 5 au sa 4 asubuhi, watu walikua wanadhani nimekufa. Sasa hili naona linaniandama hadi sasa. Nilipokua nasoma shule ya bweni, naambiwa nikae prep hadi sa 4 ilinishida, sa 2 tu nishaenda kulala au nalala darasani.

Angawaje nawahi kuamka hata kama nikilala sa 10 ikifika sa 12 lazima niamke ila hii ya kuwahi kulala inaniboa sana.

Naweza kua mahala labda Bar ingawa sinywi pombe kwa ajili ya kubuy time ili nisiwahi kulala ila muda wote nahisi usingizi.

Naombeni msaada wa natural remedies au hata over the counter medications.

Ahsanteni sana.
kunywa kahawa au vitu vyenye caffein utakuwa mlinzi kabisa
 
Nenda kwenye kituo cha afya upate ushauri wa kitaalam na tiba kama ina unalazima.
 
[QUOTE="a.hapa ndipo unapokosea

Naweza kua mahala labda Bar ingawa sinywi pombe kwa ajili ya kubuy time ili nisiwahi kulala ila muda wote nahisi usingizi.
 
Inawezekana una kisukari. Unapokula vyakula vya wanga hufanya carbohydrate kujaa kwenye damu. Kwa kuwa mwili wsko hauna insulin ya kutosha kubadili carbohydrate basi mwili hupata fatigue na kukufanya ujaribu kulala. Jaribu kutokula vyakula vya wanga kwa siku tatu mfululizo uone hali yako inaendekeaje. Ukipata nafuu nichek inbox.
 
Wakuu, habari za wakati huu.

Nimekuja kwenu kuomba msaada wa dawa ya kupunguza kulala.

Nalala mapema sana, naweza kulala sa 1, sa 2 au hata sa 12 kama nimewahi kurudi nyumbani.

Nahitaji dawa angalau ya kuniweka macho angalau hadi sa 4 au sa 5 usiku. Hii ya kulala mapema inanikwaza sana. Nilipokua mdogo nilikua naweza kulala hata kuanzia sa 11 jioni. Na nilipokua mdogo zaidi naambiwa nikilala sa 11 jioni nitaamka kesho sa 5 au sa 4 asubuhi, watu walikua wanadhani nimekufa. Sasa hili naona linaniandama hadi sasa. Nilipokua nasoma shule ya bweni, naambiwa nikae prep hadi sa 4 ilinishida, sa 2 tu nishaenda kulala au nalala darasani.

Angawaje nawahi kuamka hata kama nikilala sa 10 ikifika sa 12 lazima niamke ila hii ya kuwahi kulala inaniboa sana.

Naweza kua mahala labda Bar ingawa sinywi pombe kwa ajili ya kubuy time ili nisiwahi kulala ila muda wote nahisi usingizi.

Naombeni msaada wa natural remedies au hata over the counter medications.

Ahsanteni sana.

MREJESHO.

Wakuu, nawashukuruni sana mlionishauri nitumie kahawa.

Kabla sijatoka ofisini sa moja hivi kasoro nikamuomba mama mhudumu wa ofisi aniandalie kikombe cha gawaha ila mara moja zaidi ya kipimo cha kawaida.

Toka nimefika nyumbani sa moja niko sebuleni natazama tv wala sijahisi aina yoyote ya usingizi kitu ambacho sio kawaida kabisa kwangu, ningekua nishalala sebuleni au kuhisi kwenda kulala muda mrefu sana.

Itabidi niweke kahawa kama kinywaji changu rasmi kunywa masaa kadhaa kabla ya kulala ili niwe nakua macho angalau hadi sa 4 au 5.

Ahsanteni sana. Karbuni tuangalie televisheni.
View attachment 1003839
Kunywa energy yenye kiwango kikubwa Cha cafein

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kula Codeine phosphate 30mg Kuanzia Uchovu Maumivu viungo kulegea hamu ya kula mzigo inakomesha vyote..kuna jamaa yangu leo ana miezi sita Ngangari ni vibaya.
Ngoja na mimi niijaribu hii japo sina tatizo la kulala, nataka nipunguze masaa ya kulala kutoka tisa mpaka sita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom