Msaada wa engine ya Nadia D-4

baraka muyabi

Senior Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
162
Reaction score
58
Habari wana jamvi wenzangu...nilikua naomva msaada wa kiufundi katika engine ya gari aina ya Nadia. Inachanganya sana oil na petrol yaani naweka lita 3 za engine oil ila baada ya wiki moja namwaga lita 6 mpaka 7 (maelekezo ya fundi nimwage kila baada ya wiki)...fundi kasema tatizo ni pump..nimebadili pump nikaweka mpya bado tatizo ni lile lile. Inawaka kwa siku moja siku ya pili haiwaki..inatoa moshi mweusi ajili ya kuchanganya oil na mafuta.sasa fundi kaniambia nibadili kabisa engine niweke 3-S , kiukweli simuamini tena fundi maana nimeumia vya kutosha na tatizo haliishi..msaada tafadhali je ni kweli kubadili engine ndio suluhisho au..Nawasilisha
 
duh kumwaga oil kila baada ya wiki???[emoji15] [emoji15]
 
may be piston ring zimeisha (tatizo la moshi) ila mimi si fundi
 
Ameshapata engine huyo mafundi wa Bongo ziro kabisa wanatengeneza magari kama wanapiga ramli vile
 
ila hzo engine za 3-s ndo umemaliza kabisa shida zako zote! achana na D-4
 
Uyo fundi ina maana hana fundi mwenzake wa kushauriana nae[emoji5]????!!!! Mpk anakuingiza gharama kiasi hicho.....?!!! Hzo engine za D-4 uwa zna Tania ya kufa iyo d-4 yenyewe na kuruhusu mafuta yaingie kwenye njia ya oil ndio maana unaweka oil lita 3unatoa lita 6 kwaiyo hapo kwa ushauri wangu a check iyo d-4 kwanza kabla ya kununua engine ya 3s
 
Wataalam msaidieni huyu na wengine tuliomo humu, hasa linapokuja suala la injini ya D-4, nadia, Brevis, alion.
 
Baraka, mafundi wengi hawana uchungu na mali ya mteja. Wao wanachojali ni kuingiza siku. Wengi wanataka urudi kesho na kesho kutwa.

Nadhani baada ya kuchemka, alienda kuomba msaada kwa mafundi wengine, ndiyo maana akakwambia ubadili engine. Off which yupo right kabisa.

Ukitaka hiyo issue iishe kabisa, nunua engine ya 3S, nadhani kwa sasa itakuwa kwenye 1.6m ambayo ni complete pamoja na vikorokoro vyake. Au unaweza kununua "mswaki", ambayo ni engine tu bila makorokoro yake kama vipipe na kadhalika. Nashauri ununue complete.

Ikiwezekana nunua kwenye maduka wanayoagiza kutoka nje ya nchi kama beforward. Usije ukauziwa engine ambayo imefanyiwa overhaul.

All the best mkuu.
 
Shukrani mkuu ngoja nijipange maana nimeumizwa mpaka akili imenikaa sawa
 
Kaka pole sana...mi pia mwaka 2009 niliagiza premio iliyokuwa na d4_engine kiukweli baada ya muda ilinisumbua sana nakumbuka nilinyeshewa mvua pale mataa ya changombe sitasahau...but fundi wangu alinishauri nikanunua 3s-fe engine pale shauri moyo pamoja na control box ingine goma likarudi barabarani tena safi kabisa hadi nilipoiuza 2014 ...kwa hiyo option ya kubadili ingine ndio sahihi...
 
Kama upo dar njoo gerejini kwangu ukonga banana nikutatulie tatizo lako nimeshakutana nakesi hizo marakibao nakila niliemtengenezea hakurudi natatizo hilo tena
 
Kama upo dar njoo gerejini kwangu ukonga banana nikutatulie tatizo lako nimeshakutana nakesi hizo marakibao nakila niliemtengenezea hakurudi natatizo hilo tena
Nashukuru kwa ushauri ila nipo Mwanza mkuu...
 
Mnao mshauri kuwa aachane na hiyo engine na nyie ni mabashite tuu na vichwa maji.

Mkuu pole sana sana sana sana.kwa upande wangu mm nakuonea sana huruma aisee.hiyo unayotaka kufanya haikubaliki huwezi ingia garama ya zaidi ya milioni kwa usawa huu wa magufuri tena garama hiyo na kuliharibu gari lako maana alicho kushauri na wanachokushauri wadau hapa cha kuweka engine ya 3s ni uharibifu wa gari kabisaa.na utaingia garama mara 2 ya kununua engine nyingine ya d4.

Kurekebisba huo ugonjwa garama yake haizidi hata laki 2.

Kwenye gari yenye engine ya d4 sehem ambayo kwa asilimia 99 huwa inafanya mafuta kuingia kwenye engine na kuchanganyikana na oil ni kwenye d4 pump .

Jaribu kupeleka gari gereji nyingine au tafuta fundi mwingine pia.ili aweze kutatua hilo tatizo lako ni tatizo dogo sana lkn ukisikiliza ushauri wa kununua engine nyingine itakuumiza ww na kama unanunua basi kanunue hata half engine a.k.a mswaki tuu.kama hiyo itakuwa ishaharibiwa na mafuta
 
Hio engine ni D4 or D4 vvti? Kama una uezo kununua engine ya 3S ndio solution ya uhakika Kibongo bongo, pia ukipata d4 at a good price take it, mana d4 inahitaji matunzo, ukiijulia hata Mafuta inatumia Kidogo Kiliko 3S...tatizo lako ni dogo na linatengenezeka ukipata Fundi Mzuri na ukawa mvumilivu (Mm hua yananishinda mana mafundi wengi wababaishaji, una change Spares Moja bada ya nyingine mpaka Tatizo lipatikane)
Kutengeneza Inaweza kutengenezeka ukimpata Fundi Mzuri, ondoa Shaka, Hio ni pump or seals ..mara nyingi D-4 huharibiwa na oil Nzito tunazoweka pamoja na Mafuta ya kuchakachuliwa... Nashauri kwa d4 utumie synthetic engine oil na Mafuta P. Stations zinazo aminika
 
Shukrani mkuu LEGE ngoja nilifanyie kazi ombi lako maana huu usawa kupata milioni unatambika usiku mchana ..na bado usawa hausomi
 
Shukrani mkuu LEGE ngoja nilifanyie kazi ombi lako maana huu usawa kupata milioni unatambika usiku mchana ..na bado usawa hausomi
Mkuu, tulizana akili ndiyo uchukue maamuzi. LEGE ametuita mabashite, lakini mimi nimezungumzia experience.

Baada ya gari ya jamaa yangu kuwa na tatizo kama lako, tulimshauri aweke engine ya 3s.

Alipoenda garage, fundi akamshauri anunue engine nyingine ya D4 kwa sababu ni rahisi. Alinunua na gari ikawa fresh. Baada ya miezi kama saba hivi, issue ikaibuka tena.

Mwisho wa siku jamaa yangu aliweka engine ya 3s. Mpaka leo gari ipo fresh.

Gharama alizotumia kutengeneza, ukijumlisha kununua engine ya D4, ambayo ilifaa kwa muda, ilikuwa ni hasara tupu.

Kama ukijikunja ukanunua engine ya D4 au 3s hakikisha unanunua ya kutoka nje ya nchi. Ni sawa sawa hiyo engine yako uivue halafu ifanyiwe marekebisho kidogo na iuzwe kama used.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…