baraka muyabi
Senior Member
- Aug 13, 2012
- 162
- 58
Habari wana jamvi wenzangu...nilikua naomva msaada wa kiufundi katika engine ya gari aina ya Nadia. Inachanganya sana oil na petrol yaani naweka lita 3 za engine oil ila baada ya wiki moja namwaga lita 6 mpaka 7 (maelekezo ya fundi nimwage kila baada ya wiki)...fundi kasema tatizo ni pump..nimebadili pump nikaweka mpya bado tatizo ni lile lile. Inawaka kwa siku moja siku ya pili haiwaki..inatoa moshi mweusi ajili ya kuchanganya oil na mafuta.sasa fundi kaniambia nibadili kabisa engine niweke 3-S , kiukweli simuamini tena fundi maana nimeumia vya kutosha na tatizo haliishi..msaada tafadhali je ni kweli kubadili engine ndio suluhisho au..Nawasilisha