Msaada wa final year project title kwa bachelor degrees

Kama wanavyosema kuwa kila mtu anataka kumtengeneza hizo Patient Information Management Sytems.....
Lakini hizi kwa sasa ni zinakuwa phased out huko kwenye nchi zilizo endelea sababu ni manual standalone systems....kwamba Daktari au Nesi anachukua vipimo, halafu anaingiza kwenye systems manually...

Tengeneza project za kuwezesha automated patients information system..

Mfano mtu anachukuliwa vipimo au mgonjwa ana kuwa kwenye 24hrs monitoring wodini na vifaa tiba ambavyo vinapeleka data moja kwa moja kwenye huo mfumo wa Patient infomation system...hii ni kwa kutengeneza kitu kinaitwa HL7 Intergation Engine...ambayo inakuwa na uwezo kutoa data kwenye vifaa tiba tofauti ambavyo vina HL7 inteface....
Na huo mfumo wa Patient Infomation Management unakuwa na uwezo wa kutuma taarifa za mgonjwa kwenda kwenye vifaa tiba na kuwezesha uhakiki taarifa sahihi za mgonjwa kama ID number au dozi ya dawa...

Au tengenza PACS system( Picture Archiving and Communication System) mtu ana chukuliwa X Ray, CT au Ultrasound, halafu hizo picha za mfumo wa (DICOM image) zinakuwa zinaenda kwenye huo mfumo wa Patient Information System automatically .....

Vifaa tiba vyote vya kisasa hata kutoka China , vinafuata mfumo wa kanuni za HL7(Health Level 7 OSI model) au DICOM (Digital Imaginging and Communication in Medicine) ambazo zina unawezo wa mawasiliano na hizi Patient Information System.

Mimi sio mtaalamu wa IT, kama unaelewa ninachosema, hiyo project unaweza hata kuipeleka mahospitalini na ikafanikiwa....


Unaweza kuiita hiyo Project yako Electronic Health Records EHR au Electronic Patient Records EPR, haya ndio majina ya hizi systems zinavyojulikana huko zilikotoka....na ikiwa na mafanikio ya kutumika mahospitalini hapo unaweza hata kuiita jina lako mwenyewe....
 
Shida cost mzee....kuanza kununua vifaa tiba kwaajili ya demonstration tu , muda uliopo, na Target kwa sasa
 
Shida cost mzee....kuanza kununua vifaa tiba kwaajili ya demonstration tu , muda uliopo, na Target kwa sasa
Kwani huwezi kwenda hospitali kubwa za mkoa au kama upo Dar, Muhimbili au Mlongazila, kwenye idara ya matengenezo ya vifaa tiba au IT na kuomba kutumia vifaa tiba vyao kujaribu project yako...you will only need standard Patient Monitor for HL7 integration testing ...
Unaweza kukuta vifaa vimerundikwa vibovu kwa tatizo tofauti ila vina uwezo wa kuwaka na kuviseti kwenye demo mode ya kutransmit data....
Pole sana bongo nyoso.....Kila la Heri...
 
Kuna muda degree zinachosha sana hata mm wakat wa research nilitamani hata sijui nifanyaje
 
Inashangaza sana kuona computer engineer anatengeneza mfumo wa library!!
 
Kijana maana ya project unaijua lakini?,huwa tunapewa hiyo ili kutumia ufahamu tulioupata kutatua problems za jamii na usishangae baadhi ya projects zikiwa nzuri huchukuliwa na kuendelezwa ndo maana tuna mifumo bora na inatumika hadi sasa mfano hai ni GoTHoms inayotumika karibia vituo vyote vya afya vya umma ni mazao ya ideas za vijana wa kitanzania sasa tukupe title tukupe na source codes ukameze upresent ujinga alafu utafutiwa connection tena uingie kazini ufanye ujinga then upande cheo tena uwatumikie waliokupa connection katika kufanya ujinga mimi ningekua na mamla kwa kozi kama za kwetu hizi za ICT ningefuta kabisa course works za nadhalia na makaratasi vijana wakaanza kutafuta course works kwa practical za computer labs hata kama chuo kina computer kumi vijana wangegawanywa kwa makundi hadi zoezi likamilike miez minne ya semester ni mingi kuliko kupata wasomi wa hovyo kama hawa mimi mwenyew nafaham ugumu wa haya maswala na ni mhitimu wa chuo X pia katika kada hii hii lakini chuo chetu sikuwahi kuona kikirusu vijana wazembe ambao hata ofisi za wahadhiri hawazijui wanakimbilia huku ata wakipewe assignments unafahamu nini maaana ya superviors wako? Na unajua majukumu yake na msaada wake au unakimbilia huku IT gani wa hovyo kiasi kile ungesimamiwa na pHD kama iliyonisimamia mimi ungepigwa hata bakola swaini
 
We embu toa wazo lako sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…