Msaada wa fundi mzuri wa Nissan Dualis

KHA! YAN ule Mkopo 18M tuliokupitishia hapa HR ndio ukaenda kununua Nissan
Pumbafu kabisa hukuona Toyota wanaProduct nyingi ambazo zipo durable ununuwe!
[emoji1787][emoji1787]
 
Ndio ninaowatafuta mkuu
 

Boss una nissan unapeleka gari garage za chini ya mti? Utabadilisha kila kitu ukimfuata fundi asiemzoefu kumbe ni ishu ndogo sana..nenda kwa dealer wa nissan..
 
Boss una nissan unapeleka gari garage za chini ya mti? Utabadilisha kila kitu ukimfuata fundi asiemzoefu kumbe ni ishu ndogo sana..nenda kwa dealer wa nissan..
Nashukuru sana kwa ushauri
 
haya haya hayaaaaaaa....kumekucha
 
Gari ndogo za Nissan, VW, Audi, Pajero, Volvo, ni Kero Tanzania. Epukana Nazo. Vipuri ni shida,ni ghali, mafundi hawayajui Namna ya kuyatengeneza.
Sasa hapo tatizo ni hayo magari au tatizo ni jamii kukosa mafundi wac hizo gari.
 
Kuna maswali naomba nikuulize mkuu.

1 . Gari ulipoichukua/kununua ilikuwa na total milage ngapi?!
2. Una history ya gear box hydraulic service?! Kama ndio ni aina gani ilitumika na wewe unatumia ipi?!
3. Gari yako unatumia mwenyewe au kuna mtu mwingine huwa anaigusa.

4. Gari una muda gani nayo mikononi mwako, na je servicing huwa unafanya kwa wakati au hadi check engine light iwake?!
 
zimepakiwa nyingi tuu mjini zimepungua sanaa tuliwambia
Ni ishara kuwa wanaoziendesha ni watu careless. Kama watu hawawezi kusimamia mahusiano yao na wapenzi wao au biashara siwezi kushangaa wakishindwana na hii gari.

Dualis inataka watu makini wanaofuatilia afya ya gari 24/7.

Hii gari zipo ambazo nimeanza kuziona tokea mwaka 2010 na hadi leo zipo barabarani zina afya nzuri tu. Hakunaga gari mbovu ila kuna madereva wasio makini
 
Zimepakiwa kwa sababu gani mkuu?
Story za kuambiwa hizi. Hizi gari sasa kwa idadi zinaanza kufikia RaV4 au Harrier. Zinanunuliwa sana shida ipo kwa wazee wa kujivuta kufanya service. Mtu anataka gari ichomoke tairi ndipo apeleke service.

Gari za kampuni kama Nissan, benzi, BMW, etc utaweza shangaa unapaki sababu unavyozidi kuchelewa kuipa huduma na yenyewe inaongezeka matatizo ukienda gereji unakutana na list ya matatizo na yanataka spare replacements ambazo ni gharama kuzimudu kwa wakati mmoja .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…