Huyo si mtaalam. Huyo ni mbabaishaji. Atakisiaje gharama bila kujua eneo likoje (tambarare au muinuko), eneo lilipo ( linafikika kirahisi ?), huduma zilizopo ( maji yanapatikana?), aina ya udongo ( mchanga, ufinyanzi n.k.), huduma zitakazokuwepo ( kutakuwa na huduma ya chakula, ukumbi wa mkutano, huduma ya kufua nguo, baa n.k.). Aidha, ni ya ghorofa au ya chini?
Wateja wanaotarajiwa ni wa tabaka lipi ( wale wa 20,000 au 200,000 kwa siku)? Mwambie ndugu yako atumie sehemu ya pesa zake kupata mtaalam atakayemfanyia feasibility study kuwa ni aina gani ya hoteli italipa, atafute kiwanja, halafu apate wataalamu watakaobuni muonekano na upangiliaji wa hoteli. Ila kama anataka kujenga loji......
Amandla....