Msaada wa gharama za ujenzi wa Gest ya Vyumba 20

Msaada wa gharama za ujenzi wa Gest ya Vyumba 20

Smith Kiombo

Member
Joined
Jun 15, 2023
Posts
28
Reaction score
45
Habari zenu wana JF,

nina ombi kwa walio na utalamu wa ujenzi, nina ndugu yangu yuko nje ya nchi amejikusanya amepata pesa kiasi anataka kujenga lodge (guest house) ya vyumba 20 vyote self contained. kwa walio na uzoefu wa ujenzi ni kiasi gani cha pesa ambacho kinaweza kumaliza huo mradi?

Asanteni na karibu kwa maoni
 
Unatakiwa kuandaliwa ramani, baada ya hapo utaandaliwa estimates za materials yatakayohitajika, pamoja na ufundi.

Hauwezi kupewa makadirio ya gharama ikiwa hata ramani yenyewe hauna. Hiyo ramani ndiyo inatumika kufanya makadirio ya gharama!

Ni kazi unayotakiwa kuilipia. Ukiwa tayari nicheki PM.
 
Muhusika mkuu yuko nje ya nchi aliniambia tu wazo lake na akaniuliza ni kiasi gani ina cost but kwa kuwa siyo mzoefu ndo mana nikaja Kwenu. kama una experience na haya mambo just nipe tu idea the lowest na highest inaweza ika range kuanzia Tsh ngapi mpaka Tsh ngapi
 
Habari zenu wana JF, nina ombi kwa walio na utalamu wa ujenzi, nina ndugu yangu yuko nje ya nchi amejikusanya amepata pesa kiasi anataka kujenga lodge ( guest house) ya vyumba 20 vyote self contained. kwa walio na uzoefu wa ujenzi ni kiasi gani cha pesa ambacho kinaweza kumaliza huo mradi?

Asanteni na karibu kwa maoni
Kiwanja anacho?je ni ghorofa au bungalow
 
Unazinguaaaa njoo na kazi
Muhusika mkuu yuko nje ya nchi aliniambia tu wazo lake na akaniuliza ni kiasi gani ina cost but kwa kuwa siyo mzoefu ndo mana nikaja Kwenu. kama una experience na haya mambo just nipe tu idea the lowest na highest inaweza ika range kuanzia Tsh ngapi mpaka Tsh ngapi
Unazinguaaaa njoo na kazi, hata ukitaka ramani. njoo utapata
 
Anataka kujenga dsm ni makadirio tu ndugu hajawa na ramani ila ukiwa mtaalamu wa ujenzi ukiambiwa tu vyumba 20 self contained ni lazima utakuwa na idea ya gharama
Huyo si mtaalam. Huyo ni mbabaishaji. Atakisiaje gharama bila kujua eneo likoje (tambarare au muinuko), eneo lilipo ( linafikika kirahisi ?), huduma zilizopo ( maji yanapatikana?), aina ya udongo ( mchanga, ufinyanzi n.k.), huduma zitakazokuwepo ( kutakuwa na huduma ya chakula, ukumbi wa mkutano, huduma ya kufua nguo, baa n.k.). Aidha, ni ya ghorofa au ya chini?

Wateja wanaotarajiwa ni wa tabaka lipi ( wale wa 20,000 au 200,000 kwa siku)? Mwambie ndugu yako atumie sehemu ya pesa zake kupata mtaalam atakayemfanyia feasibility study kuwa ni aina gani ya hoteli italipa, atafute kiwanja, halafu apate wataalamu watakaobuni muonekano na upangiliaji wa hoteli. Ila kama anataka kujenga loji......

Amandla....
 
Ndo niko kwenye hatua ya utaftaji wa kiwanja
karibu kwa wazo
Fanya pia utafiti wa aina ya hoteli itakayolipa. Hoteli sio vyumba vya kulala peke yake. Ila epuka upuuzi wa kutaka kuweka zoo katika eneo la hoteli.

Na ogopa hao wanaosema watakupa ramani za ujenzi maana wengi hawana taaluma ya ubunifu majengo. Utalizwa usipokuwa makini.

Amandla...
 
Tafuta kiwanja kwanza,pia ujue kama ni ghorofa au nyumba ya chini utapata majibu kirahisi
Aanze na utafiti kwanza wa aina ya wateja anaowalenga. Kama ni maafisa au madereva kutoka mikoani, parking salama ni muhimu sana kwao kwa hiyo kiwanja kitatakiwa kiwe kikubwa.

Kama ni watalii kutoka nje, parking sio muhimu sana ila hawatataka makelele ya kitchen party. Baada ya hapo ndio atapata idea ya ukubwa wa kiwanja anachotaka utakaoendana na vyumba vya kulala na huduma nyingine.

Amandla...
 
Back
Top Bottom