ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Nilikuwa nakuheshimu sana ZeMarcopolo ila nimegundua wewe ni mtupu kabisa. Nakupuuzia na kukudharau rasmi kuanzia sasa hivi
Unanipuuzia na kunidharau kwa sababu sijakupa dawa ya figo au kwa sababu nimekwambia ukweli kuhusu swali lako la kichekibobu?
In the future unapouliza swali la kuhusu afya ya mtu specific basi usiwe mbiombio. Tulia utoe taarifa za msingi zitakazoweza kuwafanya wale wanaokusaidia kuona kuwa kweli unahitaji msaada.
Kumbuka kuwa ushauri humu unatolewa bure, ili mtu atoe ushauri inabidi awe na uhakika kuwa kweli ushauri unahitajika.
Ulipaswa kusema baba yako ana umri gani? ameumwa kwa muda gani? hospitali mmepewa options gani? ameshatumia dawa gani? hali yake kiujumla ikoje?
Ukishaandika hivyo then wachangiaji wanajua kama kuna kitu kimemiss kutoka pale ambapo umefanya jitihada, then wanajazilizia. Lakini ulichokifanya wewe ni uchekibobu kwa sababu unasema tu mzee anaumwa figo zimefail, halafu unasema umeshaenda hospitali lakini you dont bother kusema hospitali mmepewa options gani. Hayo ni matumizi mabaya ya jukwaa hili na ni dalili kwamba you dont take this jukwaa seriously...
Kuna hii thread imewekwa steaky hapo juu kwenye hili jukwaaa kwa ajili hiyo https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/382399-elimutiba-jinsi-ya-kujieleza-kwa-daktari.html