Msaada wa haraka, gari yangu imezama baharini kwa saa 24

Msaada wa haraka, gari yangu imezama baharini kwa saa 24

Gari yangu imezama kabisa baharini kwa muda wa masaa km 24 hivi ila now ishatolewa ipo nchi kavu,

Nini kifanyike plz???

Usiiwashe, ikokote mpaka gereji au mahali salama, tafuta fundi mzuri wa aina ya gari lako katika eneo lako aikague vizuri na akushauri nini cha kufanya, muhimu usiiwashe kabla ya kukaguliwa kama "imekunywa" maji kiasi gani na sehemu gani; engine, fuel tank nk ili ifanyiwe marekebisho muhimu. usiiwashe!
 
Saa 24,Baharini kuna maji ya chumvi na engine hayaendani kabisaaa! Liweke nyumbani wanao watachezea kibaba baba.....
 
Gari inapozama kwenye maji hofu kubwa ni gari kunywa maji,gari hunywa maji hasa kupitia air cleaner na maji haya moja kwa moja huenda kwenye cylinder head na hueweza kushuka chini kwenye sample.Hapa ndipo kwenye hatari kwani oil huchanganyika na maji.Lakini usisahau maji ya bahari yana chumvi na chumvi ni hatari inapoingia kwenye engine.
Sehemu nyingine maji hueza kuingia kupitia kwenye tank la mafuta.
Ushauri;
Mtafute fundi akutizamie gari yako lakini kwavyovyote hio gari cylinder head na sample vifunguliwe na kumwagwa oil yote ambayo kwavyovyote itakua imechanganyika na maji.
Pia kusafisha tank ya mafuta!
Pole na kila la heri!
 
Wataalam wanasema simu ikidumbukia kwenye maji unatakiwa uiweke kwenye nchele( mchele) masaa 24 wanasema mchele unanyonya maji yote... Nawe umesema gari limeingia kwenye maji.. Huo ndo ushaur wangu
 
Mh!! Hapo ni vingi tu vimekufa mathalani Engine sidhani kama itafaa (24 hours kwenye maji ya chumvi!)
Tenki pia la kusafisha.
Engine nina mashaka nayo uhai wake pia maana haiendani na chumvi na maji mengi yatakuwa yameingia via Air Cleaner.
Control Box itakuwa marehemu.
Dashboard pia itakuwa haifai ikianza kukauka itaanza kukatika katika...
Sasa kokotoa gharama ya hapo kwa kulifanyia ukarabati kama itawezekana (kutegemeana na majibu ya fundi wako).
Baada ya hapo jiongeze
 
Back
Top Bottom