Nimeitoa huko kwenye group.
MAPISHI YA SUPU YA MBUZI
Mahitaji:
Nyama ya mbuzi
Vitunguu maji vikubwa 2, vikate
hoho 1 kubwa, ikate vipande vidogo kiasi
njegere kikombe 1 cha chai, karot 1 kubwa ikate kate,
ngogwe/ nyanya chungu3 waweza kuzikata mara 2 au ukaziweka nzima
pilipili mbuzi 2 usizikate
viazi ulaya/mviringo 2 au ndizi 3 Vimenye osha vizuri kwa maji safi Na uvikate vipande 2
Chumvi kijiko kimoja cha kula
Maji yakuchemsha 1ltr
Matayarisho
Kata kata nyama yako
Osha vizuri Na maji safi
Iweke kwenye sufuria tia maji kiasi
Bandika nyama yako jikoni ifunike vizuri kwa dk 15
Weka viungo vyako vyote ulivyokuwa umevianda na ambavyo tayari ulikwisha vikatakata vipande
Kama supu yako itakuwa imepungua ongeza maji ya moto kiasi kulingana Na kiasi cha supu yako unayohitaji. Anagalia maji yasiwe mengi kupita kiasi. Funika kwa dk15
Epua supu yako tayari kwa kuliwa Na. Chapati, madazi au mkate [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]