Msaada wa haraka juu ya upotevu wa PC

Msaada wa haraka juu ya upotevu wa PC

high IQ man

Member
Joined
Nov 4, 2021
Posts
59
Reaction score
69
Wakuu za jioni, nilikua nasafiri kutoka kigoma kuja Dodoma na bus la AN Classic.

Nilikua na kibeg cha mgongoni

Ndani kuna PC aina ya HP kulikua kwenye carrier.

Kushuka stand naangalia kwenye beg, PC siioni ila zip imefunguliwa, nimetafta kwenye bus lote sjaona kitu,

Msaada wakuu kwenye hali kama hii tunachukua hatua gani?
 
yaani Laptop unaweka kwenye keria kisha unakaa kwenye siti na kutwanga usingizi[emoji57][emoji57]pole sana
 
Duh pole kuibiwa kitu chako INAUMA sana especially electronic devices zenye data zako muhimu siku nyingine usiweke KWENYE carrier ibebe uwe nayo muda wote pole aisee
 
Tafuta hela ununue nyingine; Next time ukisafiri PC ipakate kwenye mapaja ukishuka hotelini begi mkononi.
 
Duh, pole sana Mkuu, yaani nikijaribu kuvaa viatu vyako mpaka mwili unasisimka maana ni juzi tu nilihisi nimepoteza Camera, mwili wote ukalegea na mshtuko juu mara nikakumbuka kuwa nilihamishia kwenye mfuko mwingine.

Natamani kama kungekuwa na namna uipate lakini duh, Mwizi naye anatekeleza maagizo ya Kiongozi wake Bw Shetani a.k.a lucifer.

Ila kwa uzoefu mabasi mengi ya Arusha Dar wanatoa tangazo mapema kutokuweka begi lenye Laptop kwenye carrier, sasa siju basi hilo kwa nini hawafanyi hivyo.
 
Mkuu hatuwekag beg la laptop Kwenye keria halafu unalala usingizi, lala usingizi begi lako umelipakatia tena huo usingizi wa kufumba jicho moja
 
Mkuu hatuwekag beg la laptop Kwenye keria halafu unalala usingizi, lala usingizi begi lako umelipakatia tena huo usingizi wa kufumba jicho moja
Yaani unalala usingizi wakati mkanda wa begi umeuzungushia kwenye mikono.

Baadhi ya wasafiri wezi sana.
 
Wakuu za jioni, nilikua nasafiri kutoka kigoma kuja Dodoma na bus la AN Classic...
Kwanini bado hatutunzi mali zetu kwenye hizi public transport, kwa nn hatujifunzi? Kwenye bus unamwamini nani?

Kwanini usipakate mali yako?
 
Mimi huwa nasafiri sana na laptop kwenye kibegi na nakiweka kwenye carrier, sema mimi nafungia na nyoka. Sasa mwizi akifungua tu begi anakutana na kichwa cha 'snake', ghafla anachia na kukimbia.
 
Dodoma hapo kuna majizi ya pc sijawahi ona.
 
Mleta mada naamini hiyo laptop hukununua kwa pesa yako that's why uliweka kwenye carrier ungenunua kwa pesa yako kwamwe usingefanya kosa hilo.

Mimi begi yangu ya laptop hata nikienda kukojoa naenda nayo.

Acheni ubrazameni na ustista du mnapokuwa kwenye mabasi wezi wamejaa sana.
 
Pole sana. Ndiyo umeshaibiwa hivyo. Huna namna nyingine ya kufanya.
 
Back
Top Bottom