Hayo yote kamwambie Wakili na mtaelewana. Hapa hayatasaidia kitu
mkuu nilikua na plan hyo kwamba nitafute lawyer niongee nae tuone namna ya kufanya lakini kwa nilichokiona leo nimesita..
Nilipofika ofisi za tukta nikaingia kwenye chumba cha director kwasababu ofisi nyingi zilikua hazina watu...na director akanielezeka kwa secretary nikaingia kwa secretary na akanipatia fomu na kwakua nilikua na swali moja tu muhimu la kuuliza ikabidi nimuulize secretary kwamba
"kwakua kesi ni ya wadai wawili wenye shitaka la aina moja je pale kwenye kuandika jina nitaandika jina la nani kati yetu au nitaandika yote mawili?"
secretary akanambia "mimi kusema kweli sifahamu ila wacha nikupeleke tena kwa director anaweza kukusaidia"
tulipofika chumba cha director nikamkuta yuko na wanasheria wawili na nikaingia kuuliza swali langu tu nisaidiwe kwenye jina pale na director akanambia..
"mimi sifahamu lakini wanasheria wako hapa unaweza patana nao wakakusaidia"
sasa nikamgeukia mwanasheria na nikamuuliza swali lile lile na akanambia
"hyo iko kisheria zaidi kama unapesa naweza nkakusaidia"
hapo nikaogopa sana nikawaambia naombeni tu mnisaidie kwasababu sina pesa kwa sasa ndipo director akanambia..
"nyie vijana wa sikuhizi wajanja sana,haya bana hapo utajaza jina moja tu kwakua kesi ni ya aina moja"
basi nikamshkuru na nikaamua kuondoka ila nikapata picha kwamba mawakili wengi ni gharama na hata kama hatakukaba mwanzo lakini mwisho wa kesi lazima mtagawana hyo 3m ninayodai...hivyo nikaona bora nihangaike mwenyewe nikishindwa kabisa bas swala la wakili ndili litakua last option.