Msaada wa haraka kuhusu kukabiliana na shutuma ya wizi

Msaada wa haraka kuhusu kukabiliana na shutuma ya wizi

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
Kuna ndugu yangu alinunua mafuta yanayosadikiwa kuwa ni ya wizi kwani hakua na risiti ilionesha kua mafuta hayo ameyanunua.
Alimpatia mfanyakazi wa uwanja wa ndege ili amsafirishie kupeleka kwa bahati nzuri yakakamatwa na yule aliepatiwa kwa kusafirisha akatiwa ndani kwa siku mbili ili amtaje aliempatia mafuta siki ya tatu alitolewa kwa dhamana baada ya kumtaja aliempa na kuambiwa atowe taarifa akimuona.

Miaka 2 na nusu imepita jamaa amemuona huyu jamaa aliempa mafuta kaenda kituoni na kuchukua askari na kuemda kumkamata na wamemuweka ndani.

Sasa naomba njia na sheria ya kumpatia zamana?
Jeee njia zipi anaweza kuzitumia ili asingie hatiani?
 
Mkuu fafanua vizuri, aina ya mafuta na wingi na kadhalika.

Dhamana ni haki yake ya kisheria, kwani kosa hilo linadhamana. Cha kufanya nenda polisi na kamuombee dhamana (Polisi watakuambia mahitaji ya dhamana ili aachiwe, wanaweza kukwambia kiasi cha fedha kuweka bond au watu kadhaa wakumdhamini, hua mara nyingi wanaomba watu wawili wa kumdhamini, mmoja awe mfanyakazi wa umma na mwingine ndugu/jamaa).

Kuhusu kosa ana case ya kujibu kama uchunguzi ukikamilika na kuonesha kweli ni mafuta ya wizi. Pia ana uwezo wa kupelekwa mahakamani na kushitakiwa hata kama miaka 5 ingepita.

Makosa ambayo anaweza kushitakiwa nayo ni;

1) Kukutwa/Kusafirisha mali ya wizi. (Kama upelelezi utaonesha ni mafuta ya wizi).

2) Uhujumu uchumi/Kukwepa kodi. (Kama hawata pata ushahidi ni mafuta ya wizi basi atashtakiwa kwa uhujumu uchumi kwasababu ya kutokua na risiti ya mauzo)
 
Back
Top Bottom