Msaada wa haraka kuhusu ugonjwa huu wa bata

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Nisaidieni wadau, huo ni ugonjwa gani wa bata? Unatibiwaje?

Vifaranga vya bata wangu vinaisha kwani hupoteza uwezo wa kutembea kama muonavyo pichani kisha hufa.

MSAADA WA HARAKA WA USHAURI UNAHITAJIKA.
IMG_20220413_073704.jpg

Ninawaomba sana wana JF
 
Pole sana mkuu mm nilifuga sana bata ila nilikua nasubiri vikifika siku tatu nakua navinyonga shingo sio kwa nguvu sana ilinisaidia pia jitahidi sana wasilowe na maji km unaweza wafungia hata wikimbili kwanza wapate nguvu ndo unawaaachia ila maji wasilowe hua vinaanguka tu mpaka vinaisha.
 
Pole Sana, nimeangalia hii pichankwanza nimecheka. Hivi unampa chakula gani hicho?

Hata hivyo naomba nizungumze utunzajinwa vifaranga kwa ujumla ambalonaona ndilo tatizo lako na tatizo la wengi.

UNAWATUNZAJE VIFARANGA WAKO WA BATA?

Kuleaa vifaranga wa Bata siyo jambo dogo, wanahitaji joto zuri la kutosha ili wasipatwe na magonjwa ya baridi. Hivyo unapaswa mfugaji kuhakikisha unatumia bulbu nzuri yenye joto la kutosha #heatbulb usiku na mchana kunapokuea na baridi au mvua.

Vifaranga wanahitaji maji ya kunywa lakini hakikisha maji hayo hawayaogi ndani ya wiki 3-5 zaidi ya kunywa sababu wanaweza kupatwa na Nimonia. Andaa eneo lako la wao kushinda na kunywea maji ambalo litaruhusu maji wanayokunywa yanapomwagika hayatuami chini walipo.

CHANJO ZA BATA: Bata wakiwa ni ndege kama kuku nao wanastahili kupewa kinga. Unaweza kuwakinga na maradhi kwa kuwaweka sehemu safi. Ila kama unataka uhakika wa asilimia 200 bata wako wasife wape chanjo kwa mtiririko ufuatao.
•Siku moja hadi 6 wape dawa Neoxychick
•Siku 7 yani wiki ya kwanza (baada ya kumaliza kutumia Neoxychick) wape chanjo ya Newcastle
•Siku 14 yaani wiki ya pili wape chanjo ya Kideri
•Wakifika siku ya 21 yani wiki ya tatu wape chanjo ya Newcastle tena.
•Siku ya 24 yaani wiki ya 4, wape chanjo ya Gumboro.
Hapo utakuwa umekata mzizi wa fitina, lakini zingatia usafi pamoja na lishe bora. Inashauriwa kila unapowapa chanjo wape Vitamin kabla hujawapa chanjo ingine, na Vitamin nzuri inaitwa IntroVit A, baada ya hapo unaweza kuwapa vifaranga wapo Growers Mash bila chanjo tena na watakuwa vizuri bila tatizo.

CHAKULA CHAO: Bata hasa wakiwa wadogo inashauriwa wale starter kwa angalau kipindi cha wiki 3-4 (mwezi) na wawekewe Glucose ile ya kuku kwenye maji yao ya kunywa pamoja na Vitamin, ila kuna ambao hawafuati haya masharti.

Kuna ambao wanawanyoosha shingo bata wakiwa wadogo na bata hukua bila tatizo lolote.
 
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi!Hicho chakula ni pumba lakini hata hivyo nilikuwa nawapa mboga za majani.Kuhusu chanjo kuna mtaalamu aliniambiaga niwape chanjo ya Tatu moja nikafanya hivyo.Ajabu kuna wengine walikufa hata bila kuonyesha dalili yoyote.Huyo ha po kwenye picha anaharisha mharo wa njano na weupe
 
Hio pumba ina virutubisho? Lazima wafe tu inaonekana ufugaji sip hobby yako unafanya kuforce, Mazingira machafu kama hayo wanaacha vipikuta Typhod na kufa? Kinacho waua ni hayo mazingira machafu na kuwalisha misosi ya kipuuzi
 
Nani kwa kuambia chanjo ndo tiba? Bata wana immune kubwa sana hawawezi pata haya magonjwa ya kuambikzwa kama kideri, tatioz ni uchafu wanapata infection hasa typhod,
 
Hio pumba ina virutubisho? Lazima wafe tu inaonekana ufugaji sip hobby yako unafanya kuforce, Mazingira machafu kama hayo wanaacha vipikuta Typhod na kufa? Kinacho waua ni hayo mazingira machafu na kuwalisha misosi ya kipuuzi
Asante kwa ushauri!Ningependa unijulishe "misosi "isiyokuwa ya kipuuzi ni ipi?Wenye hobby ya ufugaji wanafugaje?Nielimishe.Pia kumbuka unaongea na mtu ambaye hajawahi fuga bata ni Mara yangu ya kwanza
 
Pole Sana, nimeangalia hii pichankwanza nimecheka. Hivi unampa chakula gani hicho?

Hata hivyo naomba nizungumze utunzajinwa vifaranga kwa ujumla ambalonaona ndilo tatizo lako na tatizo la wengi.

UNAWATUNZAJE VIFARANGA WAKO WA BATA?

Kuleaa vifaranga wa Bata siyo jambo dogo, wanahitaji joto zuri la kutosha ili wasipatwe na magonjwa ya baridi. Hivyo unapaswa mfugaji kuhakikisha unatumia bulbu nzuri yenye joto la kutosha #heatbulb usiku na mchana kunapokuea na baridi au mvua.

Vifaranga wanahitaji maji ya kunywa lakini hakikisha maji hayo hawayaogi ndani ya wiki 3-5 zaidi ya kunywa sababu wanaweza kupatwa na Nimonia. Andaa eneo lako la wao kushinda na kunywea maji ambalo litaruhusu maji wanayokunywa yanapomwagika hayatuami chini walipo.

CHANJO ZA BATA: Bata wakiwa ni ndege kama kuku nao wanastahili kupewa kinga. Unaweza kuwakinga na maradhi kwa kuwaweka sehemu safi. Ila kama unataka uhakika wa asilimia 200 bata wako wasife wape chanjo kwa mtiririko ufuatao.
•Siku moja hadi 6 wape dawa Neoxychick
•Siku 7 yani wiki ya kwanza (baada ya kumaliza kutumia Neoxychick) wape chanjo ya Newcastle
•Siku 14 yaani wiki ya pili wape chanjo ya Kideri
•Wakifika siku ya 21 yani wiki ya tatu wape chanjo ya Newcastle tena.
•Siku ya 24 yaani wiki ya 4, wape chanjo ya Gumboro.
Hapo utakuwa umekata mzizi wa fitina, lakini zingatia usafi pamoja na lishe bora. Inashauriwa kila unapowapa chanjo wape Vitamin kabla hujawapa chanjo ingine, na Vitamin nzuri inaitwa IntroVit A, baada ya hapo unaweza kuwapa vifaranga wapo Growers Mash bila chanjo tena na watakuwa vizuri bila tatizo.

CHAKULA CHAO: Bata hasa wakiwa wadogo inashauriwa wale starter kwa angalau kipindi cha wiki 3-4 (mwezi) na wawekewe Glucose ile ya kuku kwenye maji yao ya kunywa pamoja na Vitamin, ila kuna ambao hawafuati haya masharti.

Kuna ambao wanawanyoosha shingo bata wakiwa wadogo na bata hukua bila tatizo lolote.
Umeeleza vema ila kunavitu nafikiri haviko sawa,
Newcastle=Kideri=Mdondo
Huu ni ugonjwa mmoja.

Kingine sidhani kama kila ugonjwa wa kuku na bata nao wanaugua.Sijawahi sikia kama Bata nao wanaumwa kideri,gumboro haya ni maradhi ya kuku.

Uzoefu wangu kwani mimi ni mfugaji,
Bata wadogo wanahitaji starter na mult vitamin na wakikuwa kiasi wapewe dawa za minyoo,hili likifanyika sambamba na kuzingatia wanapata joto vizuri na kuwaweka mazingira mazuri vifaranga wa Bata wanakuwa vizuri na hawezi kufa kwa rate yakutisha.
Naona jamaa anawalisha machicha ya nazi hapo ndipo kwenye shida.
 
Hio pumba ina virutubisho? Lazima wafe tu inaonekana ufugaji sip hobby yako unafanya kuforce, Mazingira machafu kama hayo wanaacha vipikuta Typhod na kufa? Kinacho waua ni hayo mazingira machafu na kuwalisha misosi ya kipuuzi
Mkuu mbona umemjia kwa ukali kama mwalimu wa sayansi kimu
 
Umeeleza vema ila kunavitu nafikiri haviko sawa,
Newcastle=Kideri=Mdondo
Huu ni ugonjwa mmoja.

Kingine sidhani kama kila ugonjwa wa kuku na bata nao wanaugua.Sijawahi sikia kama Bata nao wanaumwa kideri,gumboro haya ni maradhi ya kuku.

Uzoefu wangu kwani mimi ni mfugaji,
Bata wadogo wanahitaji starter na mult vitamin na wakikuwa kiasi wapewe dawa za minyoo,hili likifanyika sambamba na kuzingatia wanapata joto vizuri na kuwaweka mazingira mazuri vifaranga wa Bata wanakuwa vizuri na hawezi kufa kwa rate yakutisha.
Naona jamaa anawalisha machicha ya nazi hapo ndipo kwenye shida.
Bata na Kuku wote wanaweza kuugua magonjwa. Japo Bata huathirika zaidi na minyoo na typhoid kutokana na mfumo wao wa maisha.

Mimi pia mfugaji wa bata ninao zaidi 150+ na vifaranga wangu wanapozaliwa kwanza huwalea mwenyewe kutoka Kwa Mama yao, hivyo hakikisha napata joto na huwapatia dawa ya Gulvet BF katika siku 6 za mwanzo na kisha chanjo ya kwanza ya Newcastle, na baadaye huendelea na chakula Starter na Gulvet.

Wakubwa kila mwezi wanapata dawa ya minyoo na multivitamin, sijawahi poteza labda kuishiwa nguvu miguu ambapo ikitokea/ imetokea Bata 2 niliwapa DCP wakapona.

Mengine Mdondo na nini nimetapata Kwa watalaamu sasa nipe shule zaidi nijifunze
 
Vifaranga wa bata wangu wamemalizikia jana. Inasikitisha sana. Kwa siku moja walikuwa wakifa wanne , watano

JESUS IS LORD
 
Umewaleaje?

Kwanza hakikisha wanapokunywa maji wanywe yakuwa na dawa, lakini wanywe tu wasiyaoge, Kwa hiyo lazima uhakikishe unawaweka.mahali ambapo hawatalowa na hiyo Unaweza kuandaa Sandusky ambalo chini linakuwa na wavu mdogo wakinywa maji mengine hutoka.pembeni ya mdomo Yao basi yasituame yapituluze chini.
 
Bata na Kuku wote wanaweza kuugua magonjwa. Japo Bata huathirika zaidi na minyoo na typhoid kutokana na mfumo wao wa maisha.

Mimi pia mfugaji wa bata ninao zaidi 150+ na vifaranga wangu wanapozaliwa kwanza huwalea mwenyewe kutoka Kwa Mama yao, hivyo hakikisha napata joto na huwapatia dawa ya Gulvet BF katika siku 6 za mwanzo na kisha chanjo ya kwanza ya Newcastle, na baadaye huendelea na chakula Starter na Gulvet.

Wakubwa kila mwezi wanapata dawa ya minyoo na multivitamin, sijawahi poteza labda kuishiwa nguvu miguu ambapo ikitokea/ imetokea Bata 2 niliwapa DCP wakapona.

Mengine Mdondo na nini nimetapata Kwa watalaamu sasa nipe shule zaidi nijifunze
Nimekupata vizuri mkuu na nimepata shule ya bure, ila hujatolea maelezo kwenye ushauri juu ya kuwapa chanjo ya Newcastle wakiwa na siku 7 na kuwapa chanjo ya kideri wakiwa na siku 14

Mdau pale juu yeye amesema kuwa Newcastle ndio kideri na kideri ndio Mdondo akiwa na maana kuwa hayo majina yote yanabeba maana ya Newcastle

Sasa je ulikuwa unamaanisha kwamba wewe huwa unawapa chanjo ya Newcastle na kideri kama chanjo mbili tofauti?
 
Umewaleaje?

Kwanza hakikisha wanapokunywa maji wanywe yakuwa na dawa, lakini wanywe tu wasiyaoge, Kwa hiyo lazima uhakikishe unawaweka.mahali ambapo hawatalowa na hiyo Unaweza kuandaa Sandusky ambalo chini linakuwa na wavu mdogo wakinywa maji mengine hutoka.pembeni ya mdomo Yao basi yasituame yapituluze chini.
Naomba picha ya Sandusky kama hutojali nataka nianze maandalizi mapema Baada ya kufiwa vifaranga wote wa bata
 
Nimejaribu kupitia comment za ushauri wa watu mbali mbali kuona jinsi gani wanavokushauri kutatua changamoto uliyonayo mi binafsi maoni yangu yako hivi
Kutokana na picha hapo tunaona vifaranga wa bata wako katika mazingira machafu napata picha kua hii ndio sababu ya yote yanayotokea inawezekana hao bata wamepata botulism
BOTULISM hii ni disorder inayosababishwa na mnyama au ndege kutumia chakula kilichokua contaminated na bacteria aitwae clostridium botulinum ambae huzalisha sumu inayosababisha kuparalazi kwa nerves ndani mwili kwenye miguu au mpaka kichwani. Hii inatokea hasa kama wametumia vyakula vilivooza au uwepo wa agents kama nzi ambao wanaleta hivo vimelea kwenye maeneo ya mifugo kutoka maeneo mengine.
Jinsi ya kuepuka ni kuhakikisha usafi wa maji na mabanda na kufanya measures za kuzuia /kupunguza agents kama nzi kwenye mabanda .

ISSUE YA CHANJO -ni kwel kua bata wanaweza kupata newcattle ,gumboro na avian pox (ndui). Lakini SIO SAHIHI kuwapatia hizo chanjo bata kwa sababu hizi chanjo tunazotumia zimetengenezwa specifically kwa aina au strain s of virus inayowashambulia kuku almost na sio bata ndo maana ni ngumu kuskia bata (local ducks )amepata Newcastle au ndui kama kuku ilivokawaida .mfugaji unapata hasara ya kuingia gharama ya kununua hizi chanjo .
NB kuchanganya bata na kuku kwenye banda moja ni hatar inarahisiha wao kuambukizana magonjwa

Magonjwa mengine yanayoweza kuwaaffect bata ni
Duck viral hepatitis huu ni ugonjwa mbaya kwa vifaranga wa bata kuanzia ndani ya mwezi baada ya kutotoleshwa unachanjo lakini tz bado azipo .

Duck viral entiritis huu unashambulia bata hasa bata wakubwa bata wanatoa kinyesi chenye rangi ya kijani yenye manjano ndani yake na mda mwingine kunakuwepo na damu .

Aflatoxins (sumu kuvu )-bata wako very senstive kwenye sumu kuvu hivo usalama wa chakula sanasana hasa kwenye pumba unatakiwa kuzingatiwa

Avian cholera (kipindu pindu cha ndege)

Collibacilosis

Ushauri
Mafanikio ya kua bata wengi wenye tija ni kuweza kucheza ni vifaranga hakikisha uwepo wa joto la kutosha kwa vifaranga usalama na usafi wa chakula na maji pia

Ushauri zaidi juu ya ufugaji kuku ,bata ng'mbe nguruwe .nk wa nicheki 0769175076

Back
Top Bottom