Msaada wa Haraka: Mama Yangu Anasumbuliwa sana na Mifupa na Presha

Msaada wa Haraka: Mama Yangu Anasumbuliwa sana na Mifupa na Presha

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Posts
1,459
Reaction score
286
Wana JF naomba msaada kwa anayemjua daktari mzuri wa magonjwa ya mifupa pamoja na presha anayepatikana hapa Dar es Salaam. Mama yangu amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mifupa, kuvimba miguu pamoja na presha kwa kipindi kirefu sasa. Tumejaribu kwenda hospitali kadhaa mkoani Mbeya lakini hali yake haijaimarika kiasi cha kuridhisha.

Naomba kwa anayefahamu daktari mzuri katika eneo hili la mifupa na presha anisaidie contact ama maelezo ya wapi anapatikana ili niweze kumpeleka mgonjwa wangu.
 
Kuumwa mifupa na kuvimba miguu na pressure si ugonjwa bt ni vihashiria vya ugonjwa fulani! Embu nijibu je katika vipimo ambavyo mama yako ameshafanya aliwah kupima "SICKLE CELL ANAEMIA"? Unaweza kutumia email yangu kama utapenda pryvas "temuerick@yahoo.com" pole mama atapona
 
Jaribu pale Regency Medical Centre, wana watalaamu wa magonjwa ya moyo.
Mpe pole mama, namuombea Mungu amjalie nafuu na kupona kabisa
 
Kwanini usijaribu physical therapy na tiba zingine mubadala?, kama ndiyo utani-PM. Pressure haitibiki hospitalini. Bonyeza link hii ukajifunze namna pressure inavyojitokeza na kujijenga mwilini.
 
Swala la mifupa,nenda PPF house ipo karibu na J-Mall maeneo ya Mtaa wa Samora Posta.Ground floor pale pana Clinic inaitwa House of Health,ni wataalamu wazuri sana wa mifupa hasa miguu,nilimchukulia hapo mama yangu dawa akapona kabisa,miguu ilimuuma kiasi kwamba halali usiku au hawezi kutembea.Pia dawa za kupunguza viashiria vinavyosababisha presha wanazo.Mshauri mama pia awe anakunywa maji ya kutosha kila siku
 
Back
Top Bottom