Msaada wa haraka: Nakaribia kufungwa

Msaada wa haraka: Nakaribia kufungwa

Ha ha ha, kwahiyo unamwambia kijana Segera inakuja!
Mtambuzi wewe hukuwahi kukopa tu-binti enzi hizo ndugu yangu!
Ndoa ya mkeka Ununio siyo utapeli, mbona hukwenda Keko!

Anyway, mleta mada msome Ngambo Ngali ameeleza vizuri.

Mimi nilisepa, na yeye akiweza asepe atakuwa ameepuka soo............
 
Habari zenu Wakuu,


Kuna rafiki yangu alinikopa laki 3 tarehe 1 mwezi November mwaka huu, tukaandikishana na kutiliana saini mimi, yeye na rafiki mwingine kama mdhamini kwani ndiye aliyenitambulisha kwa huyu rafiki mkopeshaji, katika saini hizo mkopeshaji alinitaka nimrudhie laki nne na nusu tarehe 30 Novemba yaani jana, kwa bahati mbaya mpaka jana nimeshindwa kupata hiyo laki nne na nusu bali nimempelekea laki 2 amekataa anadai nimekiuka makubaliano na kuwa kama naendelea kuchelewesha mwezi mwingine nitakuja kulipa laki na nusu zaidi yaani sasa mpaka tarehe 31 Desemba nitatakiwa kulipa laki 6 lasivyo ananifunga.


Msaada wenu jamani nitamtokaje hakimu hapa? kwani ninauhakika mpaka muda huo sina uhakika kama nitakuwa nimepata.


Msaada wenu wa mawazo jamani.
Binafsi huwa nawachukia sana watu wanaokopa halafu ikifika wakati walioahidi kurejesha, hawarejeshi au kuanza kutafuta visingizio vya kutorejesha.

Hata hivyo sioni kama anaweza "kukufunga" katika kesi hii, ingawa suala la wewe kurudisha kiasi mlichokubaliana bado huwezi kulikwepa.

Mimi nakushauri tu uwe makini hasa kama huyo mkopeshaji humfahamu vizuri. Kuna watu wengine hawana mchezo inapokuja suala la pesa. Unaweza kujikuta wewe ndio unakwenda kutafuta suluhu polisi/mahakamani na sio yeye.
 
Akienda mahakamani atasema umejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu(tapeli).lakini ni kweli deni halifungi mtu.
 
Mkuu, kwani ulitaka nikuuzie au niiweke bond? siiiuzi unakaa nayo tu kwa muda nikipata pesa nakurudishia unanipa printer yangu sikuuzii mkuu. Kwani ulitaka nikuuzie?

Kumbe ukiuza hiyo Printer pesa za kumlipa huyo mdai wako zinatimia, sasa kwa nini upelekwe mahakamani wakati kimfaacho mtu chake?
 
Back
Top Bottom