Msaada wa haraka: Nakaribia kufungwa

Ha ha ha, kwahiyo unamwambia kijana Segera inakuja!
Mtambuzi wewe hukuwahi kukopa tu-binti enzi hizo ndugu yangu!
Ndoa ya mkeka Ununio siyo utapeli, mbona hukwenda Keko!

Anyway, mleta mada msome Ngambo Ngali ameeleza vizuri.

Mimi nilisepa, na yeye akiweza asepe atakuwa ameepuka soo............
 
Binafsi huwa nawachukia sana watu wanaokopa halafu ikifika wakati walioahidi kurejesha, hawarejeshi au kuanza kutafuta visingizio vya kutorejesha.

Hata hivyo sioni kama anaweza "kukufunga" katika kesi hii, ingawa suala la wewe kurudisha kiasi mlichokubaliana bado huwezi kulikwepa.

Mimi nakushauri tu uwe makini hasa kama huyo mkopeshaji humfahamu vizuri. Kuna watu wengine hawana mchezo inapokuja suala la pesa. Unaweza kujikuta wewe ndio unakwenda kutafuta suluhu polisi/mahakamani na sio yeye.
 
Akienda mahakamani atasema umejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu(tapeli).lakini ni kweli deni halifungi mtu.
 
Mkuu, kwani ulitaka nikuuzie au niiweke bond? siiiuzi unakaa nayo tu kwa muda nikipata pesa nakurudishia unanipa printer yangu sikuuzii mkuu. Kwani ulitaka nikuuzie?

Kumbe ukiuza hiyo Printer pesa za kumlipa huyo mdai wako zinatimia, sasa kwa nini upelekwe mahakamani wakati kimfaacho mtu chake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…