Msaada wa haraka tafadhali kuhusu Western Union

Binafsi ni mteja wa Western Union Money transfer kwa zaidi ya miaka 10,mara zote hupokea PESA yangu cash,makato yote huwa ni ya mtumaji na sio mpokeaji.

Kwa hiyo kama kuna mtu anasema unatakiwa ukatwe PESA kwa kuwa ni mara yako ya kwanza kupokea PESA,naamini huo sio utaratibu wa Western Union Money Transfer.

Kila la heri!

 
Vipi kuhusu tracking fees... naona wametoa maelezo ya tracking fee na wakatoa link ili kama nataka kujua hela zangu ziko wapi nitumie hiyo link lakini nalipia...

vp hili lipogo?????
Hi,
Hakuna kitu kama hicho. Kama wewe ni mpokeaji hulipi chochote, unatakiwa uwe na MTCN namba, kiasi cha pesa ulichotumiwa, swali la mtumaji, na jibu lake. Gharama za utumaji zinalipwa na mtumaji. Huo ndio utaratibu wa Western Union.
 
Kama uko na documentation kuhusu hio $$109 nadhani ukienda na kuona bank manager waweza kupata hio pesa yako , kama hakuna document yeyote basi imekula kwako na sahau
 
Haro watu wa western union ni wezi wakubwa wengine tuliamua kuachana nao miaka mingi iliyopita tangu na baada ya september ieleven wakati walipoanza kudhulumu pesa za waislam kwa kisingizio cha ugaidi,yaani wewe siku zile jina lako likiwa ni la kiislam na anayepokea ni muislam basi ujue hela yako ilikuwa inazuiliwa kwa kutumia sababu za ugaidi wengi wamedhulumiwa kwa njia hiyo na tena charge zao za kutuma ni kubwa mno na kama huyo mtu anayetuma pesa yuko sehemu yeyote north America,siku hizi kuna kitu inaitwa money gram unaweza kutuma kwa kupitia post office yeyote ile ,hawa wako rahisi kama moja mbili tatu,na pia service charges zao ni rahisi mno kama ukilinganisha na wezi western union. Mr.Murage Msherwampamba.
 
Vipi kuhusu tracking fees... naona wametoa maelezo ya tracking fee na wakatoa link ili kama nataka kujua hela zangu ziko wapi nitumie hiyo link lakini nalipia...

vp hili lipogo?????

Hao wanakuingiza mjini mkuu, huna sababu ya kufanya tracking kwani pesa ikishatumwa; Mpokeaji anaweza kuichukua ndani ya dakika tatu!.
 

Mara ya kwanza kusikia hii tuhuma. Mkuu umewahi kuwasilisha malalamiko yako WU? That is truly a shocker. Nimetumia huduma hii kwa zaidi ya 10 yrs and is one of the safest.
 
kama unasubiri kutangaziwa utasubiri milele,hakuna tangazo la hivyo


Ha ha nafikiri lugha sahihi ungesema wewe ni mtumiaji mkubwa ungeleta utulivu Wa pragmatiki but kusema wewe ndo mtumaji mkuu ina maana sisi wote tunaotuma PESA kwa western union wewe ndo unatuongoza je ni kweli?

Ni kweli wewe ndiye mtumaji mkuu Wa PESA kupitia western union? Unatuma kiasi gani,? Kwa vigezo vipi mpaka kujiita mtumaji mkuu?
 

mimi natuma zaidi na kupokea zaidi
 
 
Vipi kuhusu tracking fees... naona wametoa maelezo ya tracking fee na wakatoa link ili kama nataka kujua hela zangu ziko wapi nitumie hiyo link lakini nalipia...

vp hili lipogo?????

Tracking fee?!!! Hebu twende taratibu kwanza, hiyo tracking fee nani kakwambia ulipe? unalipia wapi?
Unamjua anayekutumia pesa? Wasiwasi wangu isijekuwa some random dude from online amekwambia anakutumia pesa ndiyo anaomba ulipe hizo fees!!
 
kupokea pesa western union
-Jina la mtumaji na nchi aliokutumia
-kiasi
-Swali na Jibu lake ( Hivi atakupa mtumaji direct wewe)
-jaza fomu ya western union kwa info za hapo juu
-Pokea hela
-Katumie hela
-Omba utumiwe tena
-Rejea hatua ya kwanza
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…