Mkuu kwanza nikupe pole kwa yaliyomkuta Shangazi yako,hapa kuna kitu usipokiweka sawa Shangazi yako aweza kutwa na hatia.
Hivyo nionavyo mimi ni bora hiki kifanyike:-
Cha kwanza ni kukataa kosa,ikiwa atakataa kosa inabidi awe na uthibitisho usio shaka kuwa kweli hakutenda kosa hilo,yaani akane kuwa ;-moja hakuwahi kumpiga paka,mbili hajui hata kama jirani yake anafuga paka,tatu siku ya tukio kulingana na mdai ,yeye hakuwepo alikuwa sehemu nyingine ,hapa itabidi atafute hata tiketi zenye kuonesha kuwa alisafiri pia shahidi wa kule alitembelea siku ambayo mdai anadai kutendewa kosa,shaihidi huyo apangwe asijichangaye,pia watoto japo mmoja aliyepevuka kiakili aseme kuwa siku ambayo mama yake anatuhumiwa kutenda kosa hakuwepo nyumbani alikuwa kwa mtu x,au sehemu x nk.