Shemeji yangu alikuwa anaishi/amepanga kwenye nyumba za shirika la uma. Kutokana na matatizo ya kiuchumi alichelewesha kodi ya pango na hivyo shirika lile likamvunjia mkataba wa upangaji na kumpa siku 14 awe ameachia nyumba. Aliandika barua kuomba aongezewe muda michache na atalipa Kodi ama atahama siku 14 ni chache sana. Hakujibiwa barua Ile Bali shirika lilielekeza kampuni ya majembe imtoe kwenye nyumba.
Siku waliyoenda kufanya eviction walikuta watoto wawili tu nyumbani, mmoja wa miaka 10 na mwingine wa miaka minne. Walimpigia simu shemeji yangu akaomba wamsubiri anafika lkn wakaendelea na zoezi na majembe walikamata Mali zote na kuzipakia kwenye Lori na shemeji yangu alipofika waliondoka na vitu vyote kwenye Lori, aliomba APEWE orodha ya vitu walivyobeba na apewe nyaraka na nguo na vyakula lkn majembe walikataa wakisema wameshapakia vitu hivyo.
Shemeji yangu aliendelea kuomba arudishiwe nyaraka hizi ambazo ni pamoja na VYETI vya taaluma pamoja na nguo zikiwemo uniform za watoto na madaftari na vitabu vyao lkn majembe walikataa kurejesha vitu hivyo walitaka alipoe storage charged. Shemeji yangu hakuwa nayo. BAADAE majembe walimwelwza kwamba wamepata majanga ya mafuriko hivyo vitu vyake vimeharibika.
VYETI vimeharibika, nguo zimeharibika na bado ni Zaid ya miaka mitano wamekataa kumrejesha VYETI hivyo pamoja na nyaraka zake muhimu ambazo zimemfanya akakosa hata ajira.
Je katika SHERIA za eviction unaruhusiwa kumkamata nyaraka, VYETI, vitambulisho na nguo na madaftari na vitabu vya WANAFUNZI?