Msaada wa haraka wa kisheria kuhusu Sheria ya Eviction

Je unaweza kusaidia kunifahamisha kwamba eviction inapofanyika dalali anakamata vitu na KUKAA navyo ama anavipiga mnada?? Kwenye issue hii ya shemeji dalali alipakia vitu akapeleka kuhifadhi kwenye ghala yake na kuanza kucharge storage..akaombwa aachilie VYETI akagoma. Hakupiga mnada vitu mpaka akapatwa na mafuriko na Mali zikaharibika...angekuwa katoa vifaa akatupa nje vikaharibiwa ama vikaibiwa hapo sawa...lkn dalali alivichukua akapeleka store yake akaanza KUCHARGE storage...aliambiwa na nani? Ni sahihi?
 
Na je ni muhimu kupewa notice? Shemeji yangu alipewa notice ya 14 days, ahame. Ni sawa?
 
pengine wakati wanachukua vitu vya shemeji yako isingekuwa rahisi kufahamu ndani yake kuna vyeti au madaftari ya shule,ila kwa namna yoyote ile zoezi la kuchukua vitu halikufanyika kwa haki au usawa kama ulivoeleza hapo awali.
Mimi nilidhani eviction wangetoa vitu nje, hata vingeharibika ningemwambia shemeji kosa ni lako... Lakini majembe wamevitoa, wakavishikilia Ili wapige mnada Kodi ilipwe.. shemeji ameomba APEWE VYETI na nguo na documents muhimu, majembe wamegoma wanataka awalipe storage ya 400,000/ kwa siku. BAADAE kaenda Tena yupo TAYAR alipe hiyo storage wao ghala lao wanasema limepata mafuriko...kwani SI Wana bima?? Nani aliwaomba wahifadhi hivyo vitu... Na kwanini hawakupiga basi mnada wamekaa na vitu zaidi ya mwaka??
 
Poleni Sana kwa changamoto,naomba kukujibu kesho kwa umakini zaidi
 
Rudi kwenye mkataba wake kwanza
 
Yes, ni kweli.

Reasonable time for a legal eviction order is minimum of 30 days, not 14 days.
Sasa hapo wanasema kwamba mtu kama hajalipa Kodi anahesabia ni trespasser, hivyo ni mpangaji haramu hafai kupewa notice...nimeogopa sana.

Cha pili, auctioneer anapopewa order ya kufanya eviction hapo hapo anaruhusiwa kumkamata vifaa vya mteja na kuviweka ghalan kwake Huku akidai alipwe storage charges?
 
Cha pili, auctioneer anapopewa order ya kufanya eviction hapo hapo anaruhusiwa kumkamata vifaa vya mteja na kuviweka ghalan kwake Huku akidai alipwe storage charges?
sina Experience sana na practise inayofanyika na Brokers ila ambacho naweza kusema ni kwa muhiska kufika ofisini kwao kuomba mchanganuo wa gharama husika ilikuweza kujua namna ya kuendelea mbele zaidi
 
Mahusiano kati ya mpangaji na mwenye nyumba ni katika kutimiza terms za mkataba lipa kodi ya nyumba pata haki ya kuishi kwenye hiyo nyumba,mpangaji muda wa mkataba ukiisha na ukashindwa kulipa Kodi tayari wewe ni mvamizi na huna mahusiano tena na mwenye nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…