Msaada wa haraka wa kisheria.

Msaada wa haraka wa kisheria.

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
620
Reaction score
370
Wakuu salamu,
Naombeni msaada wa kisheria kuhusu suala hili.
Nimekopa benki ikafika kipindi nikashindwa kurejesha vizuri marejesho yangu kwa sababu ya kupata hasara katika biashara yangu. Nikamwomba jamaa yangu aniazime pesa ambayo nitailipa kwa riba nilipe benk ili wanipe mkopo mwingine. Ndugu yule akanipa pesa kwa mkataba lakini hakunipa yote niliyohitaji matokeo yake nikachelewa kukamilisha rejesho kwa wakati nabenki kunipiga penalt na kuninya mkopo.
Jamaa yule akadai alipe deni lote ninalodaiwa na benk na aniongeze pesa kidogo nimpe nyumba yangu. Nikakataa kwani thamani ya deni hailingani na thamani ya nyumba yangu. Jamaa yule akaenda mahakamani na mahakama ikanihukumu nimlipe pesa yake ndani ya siku 30. Nikakata rufaa mahakama ya wilaya, Kabla rufaa haijasikilizwa jamaa akazusha kuwa nauza nyumba na ninataka kukimbia. akawapigia simu watu wa benki wakaja na yeye pamoja na polisi kunikamata huku wakisisitiza wale wa benki yule jamaa awalipe ili mimi na yeye tuendelee na kesi.
Mimi nimekataa kulipiwa deni na huyu ndugu ambaye inaonekana wazi kuwa hakuwa na nia ya kunisaidia isipokuwa alikuwa na nia na nyumba yangu ambayo anataka kuipora kwa nguvu. Pia nimeanza kupata wasiwasi kuwa jamaa huyu anataka kushirikiana na benki ili alipe na achukue hati za nyumba yangu ili apore nyumba yangu.
Je ninaweza kumfungulia kesi kwa kitendo alichokifanya cha kunizushia kuwa nimeuza nyumba na kuja na maaskari usiku saa mbili na maafisa wa benki na kunikamata?
Waliponifika kituoni nikakataa mawazo yao wakatishia kuniweka ndani nikakubali wakaogopa kuniweka ndani na wakakiri kabisa habari walizoambiwa kuwa nimeuza nyumba si za kweli wakaniacha nikarudi nyumbani. Wakaniomba nijitahidi kesho nifike benki tukaweke sawa jambo hilo.
Naombeni msaada wa kisheria wakuu juu ya jambo hili.
 
Ndugu tafuta Ofisi ya Advocate kama 20 au 30 mshirikishe hiyo habari lkn humu watu wa Sheria nimara chache sana kukupa Ushauri nimefatilia humu namaanisha ninachokwambia usipoteze muda wako
 
Mahakama ya wilaya ilitupilia mbali sababu za rufaa yangu pamoja na kutojibiwa na mjibu rufani hata sababu moja.Rufaa iko mahakama kuu huku Mahakama ya Mwanzo ikiwa imetekeleza hukumu kwa kuuza Mali zangu na kumpatia mdai pesa yake na pesa iliyobaki kubaki mahakamani.
 
Pole ndugu..kwa yaliyokukuta unataabishwa sababu huna HELA na huyo jamaa yako alijua hivyo ndio maana kakufanyia uhuni..huwa nawadharau sana watu wanaotokwa mapovu eti...Mahakamani ..kuna Haki...ninachojua Mimi Mwenye Hela ndio anaamua kesi haijalishi mlalamikaji au mlalamikiwa...Yaliwahi kunikuta naongea ninachojua...Kwa issue yako ndg yangu jamaa ameshakuwahi...Nakushauri kubali matokeo kwamba umepoteza jipange Upya sababu huo muda utakaoutumka Mahakamani unaweza kuutumia kurekebisha ulipoanguka nakuhakikishia hutapata Haki yako ila kama naww una Hela kumzidi huyo jamaa sawa!
 
Tafuta wakili mzuri kama Dr. Masumbuko Lamwai aishughulikie hiyo kesi, yaani huyo jamaa atajilipa mbona.
 
duh!,walimwengu wana roho za kisheitwan sana
 
Back
Top Bottom