Kuchasoni Kuchawangu
JF-Expert Member
- Aug 21, 2012
- 620
- 370
Wakuu salamu,
Naombeni msaada wa kisheria kuhusu suala hili.
Nimekopa benki ikafika kipindi nikashindwa kurejesha vizuri marejesho yangu kwa sababu ya kupata hasara katika biashara yangu. Nikamwomba jamaa yangu aniazime pesa ambayo nitailipa kwa riba nilipe benk ili wanipe mkopo mwingine. Ndugu yule akanipa pesa kwa mkataba lakini hakunipa yote niliyohitaji matokeo yake nikachelewa kukamilisha rejesho kwa wakati nabenki kunipiga penalt na kuninya mkopo.
Jamaa yule akadai alipe deni lote ninalodaiwa na benk na aniongeze pesa kidogo nimpe nyumba yangu. Nikakataa kwani thamani ya deni hailingani na thamani ya nyumba yangu. Jamaa yule akaenda mahakamani na mahakama ikanihukumu nimlipe pesa yake ndani ya siku 30. Nikakata rufaa mahakama ya wilaya, Kabla rufaa haijasikilizwa jamaa akazusha kuwa nauza nyumba na ninataka kukimbia. akawapigia simu watu wa benki wakaja na yeye pamoja na polisi kunikamata huku wakisisitiza wale wa benki yule jamaa awalipe ili mimi na yeye tuendelee na kesi.
Mimi nimekataa kulipiwa deni na huyu ndugu ambaye inaonekana wazi kuwa hakuwa na nia ya kunisaidia isipokuwa alikuwa na nia na nyumba yangu ambayo anataka kuipora kwa nguvu. Pia nimeanza kupata wasiwasi kuwa jamaa huyu anataka kushirikiana na benki ili alipe na achukue hati za nyumba yangu ili apore nyumba yangu.
Je ninaweza kumfungulia kesi kwa kitendo alichokifanya cha kunizushia kuwa nimeuza nyumba na kuja na maaskari usiku saa mbili na maafisa wa benki na kunikamata?
Waliponifika kituoni nikakataa mawazo yao wakatishia kuniweka ndani nikakubali wakaogopa kuniweka ndani na wakakiri kabisa habari walizoambiwa kuwa nimeuza nyumba si za kweli wakaniacha nikarudi nyumbani. Wakaniomba nijitahidi kesho nifike benki tukaweke sawa jambo hilo.
Naombeni msaada wa kisheria wakuu juu ya jambo hili.