Msaada wa haraka wapendwa, mgonjwa wangu anahitaji Upasuaji MOI na familia haina fedha

Msaada wa haraka wapendwa, mgonjwa wangu anahitaji Upasuaji MOI na familia haina fedha

Status
Not open for further replies.

Bnon

Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
40
Reaction score
67
Nawasalimu ndugu zangu.

Samahani kwa usumbufu, kaka yangu alipata ajali mbaya sana ya pikipiki akiwa kwenye mizunguko yake.

Aliumia hasa, akapelekwa Taasisi ya MOI, ndugu tumepeleka hela nyingi tuzizochanga familia yetu ni duni sana zimeisha kwenye vipimo, sasa tangu Ijumaa amegundulika anashida kwenye UTI wa mgongo inahitajika milioni moja na laki sita kwa ajili ya operation.

Familia tumejichanga imefika laki tatu Tu... Na tumekopa na kukopa hadi kufikia hapo.

Sasa wamesema hawawezi kumtibu hadi pesa ilipwe hata nusu na tukiendelea kuchelewa ataoza.

Nisaidieni ni wapi wanaweza kutupa msaada yupo MOI 🥲🥲🥲🥲🥲🥲😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭.

MOI YATOA UFAFANUZI
Kujua walichojibu MOI, bofya hapa ~ Baada ya Mdau wa JF kuomba msaada Mgonjwa wake afanyiwe upasuaji, MOI yatoa ufafanuzi na maelekezo
 
Pole sana, ila ingependeza ungeweka na ushahidi wa nakala kutoka hospital(picha) ili mwenue kuguswa aweze kukuchangia chochote kitu
 
Pole sana, ila ingependeza ungeweka na ushahidi wa nakala kutoka hospital(picha) ili mwenue kuguswa aweze kukuchangia chochote kitu
Sawa ndugu yangu .. nilikua nauliza namna ya kuwapata viongozi apate matibabu maana anasiku ya 21 Leo tangu apate ajali😭😭😭😭
 
Wapendwa naombeni ushauri namna ya kupata msaada kwa viongozi wetu, kaka angu alipata ajali mbaya sana ya pikipiki akiwa kwenye miangaiko mwananchi Dar es Salaam.

Leo ni siku 21 tangu apate ajali, amegundulika anashida kwenye UTI wa mgongo umepoteza mawasiliano kabisa anatakiwa kufanyiwa operation gharama ni milioni 1.6. Familia yetu ni duni sana, yaani zaidi ya sana.

Sasa pesa imekua changamoto na wamesema hawatamtibu Hadi pesa na akichelewa atahoza .😭😭😭😭😭😭jamani msaada kwa viongozi. Tumejichanga kama familia tumepata vipimo maana vilikua gharama sana. Sasa tumefika mwisho sote tunalia😭.
 
Pole sana

Mbunge Kishimba alishauri matibabu bure kwa wote ni jambo la muhimu sana
 
Mtafute ndugu Godlisten Malisa ana platform kubwa na ushawishi mkubwa kwa jamii endapo atpokea ombi lako mawwza pata msaada huo ndani ya masaa tu
 
Pole sana

Mbunge Kishimba alishauri matibabu bure kwa wote ni jambo la muhimu sana
Asante... Naona nikimpoteza Kaka yangu kwa umasikini wetu. Natamani kupata viongozi watusaidieeeee
 
Mtafute ndugu Godlisten Malisa ana platform kubwa na ushawishi mkubwa kwa jamii endapo atpokea ombi lako mawwza pata msaada huo ndani ya masaa tu
Kaka naomba direction naweza kumpataje nimetafuta contact zake nimrkosa... Msaada Kaka🙏
 
Wacheki bodaboda wenzake naonaga wana umoja sana barabarani wanaweza kuonyesha pia mshikamano kwenye hili. Ahsante
 
Kiufupi Hadi sasa wamesaidia sana.... Kaka ... Lakini pesa ni nyingi .. ata hapa tulipofika wameungana nasi... Maana familia yetu ni zaidi ya duni Kaka.
Wacheki bodaboda wenzake naonaga wana umoja sana barabarani wanaweza kuonyesha pia mshikamano kwenye hili. Ahsante
 
Ok asante Kaka... Vyote tumeshafanya lakini bado Hali ni ngumu.... Familia ni masikini sanaaaaa ndugu yangu.. aisee🙌🙌🙌
 
Kuna wa mama wanapitaga kutoa Chakula kwa Wagonjwa Ni wamama wa Kiislam. Hao watapo pita ongea na mmoja akufikishie swala lako kwa moja ya watu wanaowafahamu wawalipie hata robo bili inayotakiwa wanaeza kukusaidia.

Huwa wana tamaduni za kupelekea bili baadhi ya matajiri wengi wa kariakoo ambao ni Waislam na wanazilipia.. KWENYE SWALA LA UTU WAISLAM WANAJITAHIDI SANA KUSAIDIA WATU MAHOSPITALI
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom