Msaada wa hizi spare kwenye gearbox

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,286
Reaction score
39,418
Wanajukwaa habari, naomba msaada wa hzi spare za gearbox gari yake ilikua ma shida hivo baada ya kwenda kwa fundi kuicheki wakakuta hivi vifaa ni vya kubadilisha.

nock sensor, shift gear na gearbox sensor, na pump. Kwa anaejua bei zake za mtumba tunaomba msaada, bei alizotaja fundi ni balaa.



 
Nunua tu gearbox used nyingine,ukinunua kimoja kimoja hutaokoa kikubwa,nafikiri gear box ya IST ni 1M to 1.3M

Fundi amesema haina haja ya kubadili coz anafanya service ya gari hvo ndo vya kibadilisha ila gearbox haina shida ilikua inapiga kazi vzr tu, ila fundi kashauri hizo parts zibadilishwe
 
kwa ushauri mdgo tu naweza kupa bei ila itakuwa n kulingana me napata vp spare ukakuta mambo n tofauti cha muhmu hapo nenda ilala upande wa spare au tandale fanya window shopping mwywe jipime den ingia ktk manunuzi
 
Fundi amesema haina haja ya kubadili coz anafanya service ya gari hvo ndo vya kibadilisha ila gearbox haina shida ilikua inapiga kazi vzr tu, ila fundi kashauri hizo parts zibadilishwe...........................Siku zote Mafundi huvutia upande wao!,

Ameshajua ukipata suluhisho, nae utampa kwaheri mpaka mwakani ama ndio bye bye...nunua Gear Box nyingine mtumba, na umalize hio biashara kabisa!!!
 
Mleta uzi usikubali huyo fundi aguse hiyo gearbox.Kama ni fundi hodari wewe endelea kuendesha gari yako hadi hapo hiyo gearbox itakapoharibika halafu mpelekee aitengeneze.Kwa sasa kama gearbox ni nzima asiiguse.
 
Kwanini usijichange kidogo tu mkuu ukanunua gearbox used?kwa uzoefu wangu,hizo spare utazipata,gearbox itarudishiwa,lakini usifikiri itarudia hali yake ya kawaida...
 
sasa anapaswa kufanyaje mshaurini kabla Hajarud tena umu
Mkuu wewe unataka tumshauri nini?

1. Amekiri mwenyewe kwamba gearbox ni nzima.

2. Vitu vinavyohitaji preventive maintenance kwenye gari vinafahamika.

Kwenye gari hata siku moja haitokaa itokee solenoid valves ziwe timed preventive maintained. Solenoid kwenye gari ni kama Hizo solenoid valves zote za gearbox, VVT solenoid, VSV solenoid, SCV solenoid pamoja na relay zote

Kitakachokufanya ubadili solenoid ikiwa bado zinafanya kazi ni kama tu zitakuwa na resistance ambayo ni nje ya ile ambayo inatakiwa kuwa nayo.

Mfano hii ni screenshot ya kipande cha manual book ya gearbox mojawapo ya toyota. Sitosema ni gearbox ya gari gani.



Hapo wameonesha connector ya gearbox na pin zake na wakasema kwa kila solenoid valve resistance inatakiwa kuwaje. Hapo ndio umuhimu wa repair manual unaingia.

Kwa mfano Pressure control solenoid inatakiwa kuwa na resistance kati ya 4.5Ω mpaka 6Ω.

Kama ukipima na multimeter ukaona iko nje ya range badili solenoid. Hili halina mjadala.

Na katika hali ya kawaida gearbox haiwezi kuuza solenoid zote hata kama utatoa oil na kuweka maji.

Bado namtakia kila la heri mtoa maada. [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kuna fundi bwege bahati yangu nilimnote kabla hajaigusa gari,nilienda kwake na shida ya kugonga mguu mmoja wa nyuma,wakati tunatest akaniambia "halafu hii gari haijatolewa thermostat,inabidi tuitoe hii sijui sababu yake ni kwa nchi za baridi",aliposema hivyo nikamshusha hapo hapo fala yule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…