sasa anapaswa kufanyaje mshaurini kabla Hajarud tena umu
Mkuu wewe unataka tumshauri nini?
1. Amekiri mwenyewe kwamba gearbox ni nzima.
2. Vitu vinavyohitaji preventive maintenance kwenye gari vinafahamika.
Kwenye gari hata siku moja haitokaa itokee solenoid valves ziwe timed preventive maintained. Solenoid kwenye gari ni kama Hizo solenoid valves zote za gearbox, VVT solenoid, VSV solenoid, SCV solenoid pamoja na relay zote
Kitakachokufanya ubadili solenoid ikiwa bado zinafanya kazi ni kama tu zitakuwa na resistance ambayo ni nje ya ile ambayo inatakiwa kuwa nayo.
Mfano hii ni screenshot ya kipande cha manual book ya gearbox mojawapo ya toyota. Sitosema ni gearbox ya gari gani.
Hapo wameonesha connector ya gearbox na pin zake na wakasema kwa kila solenoid valve resistance inatakiwa kuwaje. Hapo ndio umuhimu wa repair manual unaingia.
Kwa mfano Pressure control solenoid inatakiwa kuwa na resistance kati ya 4.5Ω mpaka 6Ω.
Kama ukipima na multimeter ukaona iko nje ya range badili solenoid. Hili halina mjadala.
Na katika hali ya kawaida gearbox haiwezi kuuza solenoid zote hata kama utatoa oil na kuweka maji.
Bado namtakia kila la heri mtoa maada. [emoji16][emoji16][emoji16]