Msaada wa hospitali inayofanya IVF kwa Tanzania

Mavindozii

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2012
Posts
2,111
Reaction score
2,781
Wakuu wa nchi naomba kuuliza, kama Kuna mtu anayejua hospital inayofanya hiyo IVF kwa hapa Tanzania msaada please.
 
Wakuu wa nchi naomba kuuliza, kama Kuna mtu anayejua hospital inayofanya hiyo IVF kwa hapa Tanzania msaada please.
Ipo moja Mikocheni, ina bango lake barabarani. Ukiwa unatokea shopperz Plaza kama unakwenda Kawe, ukishapita shoppinga mall moja hivi mkono wa kulia kuna bango lao, jina siifahamu, nadhani kuna wadau watakupa jibu.
 
In vitro fertilization sidhani kama kuna hospital wanafanya umasikini huu ndugu yangu vitanda tu raisi ameshindwa unategemea nn jaribu kwenda nairobi
 
Nenda tumaini hospital upanga, kamwone dr Amri,ameanzisha huduma ya IVF,,,gharama yake ni dollar 5000..
 
Mdadamwema,dollar elfu 5000, mbona ni nyingi kwa sana,wenye uhitaji wa hilo tatizo watapata huo msaada kweli?
 
Ndo hivyo mkuu,IVF ni gharama sn,yaani mpaka ujipange kisawasawa,na ni bora huyo drAmri ni dolla 5000,kuna hiyo clinic iko mikocheni inaitwa Dar IVF Center,ni million kumi na sita.
Nairobi IVf center kidogo wako chini ni dollar 4000,ila ukichanganya na hiyo nauli kwenda kurudi pia gharama za hotel kwa siku zisizopungua kumi na tano,nikaribia tu na hiyo dollar 5000.Maana unatakiwa ukae huko kwa muda usiopungua wiki mbili ukipatiwa matibabu ya kuyutubisha mayai chini ya uangalizi maalum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…