Msaada wa Imani

Kwasababu ni kitabu cha kiroho sio hadithi
Kitabu cha kiroho ambacho sio kutoka kwa Mungu?
Hivi neno la Mungu linaweza kua na makosa au kuwa na Contradiction?
Hua napenda kutumia mfano mdogo sana wa KIFO CHA YUDA kuonesha wazi biblia inamikono mingi ya wanadamu yaani imebadilishwa sana. Na kitabu kilichabadilishwa hatuwezi kukiamini. Kitabu cha Mungu Hua hakiwezi kutiwa mikono ya waandishi.
Sasa wewe kaa na hiyo Biblia ukidhani ni ya Mungu. [emoji23] [emoji23]
Au kama unabisha kua haijabadilishwa niambie Yuda alikufa kifo Gani?
 
Halafu mi nahisi nafanya mjadala na mtu asie na akili timamu. Kumbe naweza kua napoteza mda wangu bure kwa mtu asie na akili za uelewa. Akili zako zinaonesha wazi huelewi chochite ila umekaririshwa na umepandikizwa chuki kubwa! Kila nikikuuliza ushahidi wa unachokisema haujibu unazidi kuleta kashfa. Sasa kama unataka tuendelee mjadala naomba jibu maswali yangu na uliza ya kwako . Kama huwezi itaonesha wazi hujui lolote ila unadhani unajua. Sasa please kama imeshindwa kujibu tulia acha wanaume tuendelee na mada na wewe nenda jikoni kapike.
 
Sidhani mnajua mnachobishania,mungu ni wengi mno kuna Yahweh, Allah na wengine kibao so hawafanani hata kidogo.
 
Tupe elimu
Elimu sikupi,ila ushauri tu.Shikamana na huyo Mungu uliyeshakabidhiwa kwake,mjue sana na umpende kwa moyo wako wote na mafundisho yake uyashike.wa jirani mwachie mwenyewe akiona wako ni mzuri atakuja kumtafuta.mungu naye anapigiwa debe kama daladala.
 
SUBUHANA LLAH, INNA LILLAHI WAINA ILAYIHI RAJIUUN
 
Habari wana JF. naomba kufahamishwa kuhusu Yesu Mtoto wa Mariam. Je Imani ya Wasabato, Waroma na Madhehebu mengine wanamchukulia kama Nani? Je ni Mungu? Mwana wa Mungu ama Mtume wa Mungu? Asanteni.
Naomba nifafanue japokuwa jibu lake litakuwa gumu kumeza haswa kama huamini biblia na huamini Uungu wa Yesu Kristo. Cha kwanza kabisa naomba niseme bila uwoga kwamba Mungu ni mmoja hii inafafanuliwa kiundani kabisa katika biblia japo naomba nikupe mstari wa kuipa uhai dai langu hili shupavu. Tukiangalia katika Kitabu cha Isaya 45:18 inasema
"For thus saith the LORD that created the heavens GOD Himself that formed the earth and made, He hath established it, He created it not in vain, He formed it to be inhabited I AM the LORD and there is none else"
Katika mstari huu mwanana tunapata kwanza uelewa kuwa Mungu ndiye Muumbaji na Yeye ndiye aliyeiweka hapa ilipo mbingu na nchi vyote Yeye ndiye aliyevifanya viwepo na pia Hakuiumba bure bure tu ila Aliiumba ili viwepo vitakavyoijaza na cha mwisho ni kuwa Yeye ndiye Mungu na hakuna mwingine.
Baada ya hayo naomba sasa tuje kwenye Uungu wa Yesu Kristo na hapa ndipo ukakasi mwingi ulipo na kwa kupitia huu uzi naona kuwa wewe mheshimiwa kwamba Injili ya Yohana unaijua lakini unaisoma kwa mtazamo ambao kidogo sio mzuri na nnajua kuwa nikileta mstari kutoka huko swala la Yesu kusema Baba litazua mtafaruko basi tufungue waraka kwa Waebrania 1:8-10 ambapo Baba anaongea na Mwana na ninadhani kwamba mwenzangu ushajua kuwa Mungu ndiye Baba na Yesu ndiye Mwana basi waraka unasema hivi....
"8. But unto the Son he saith, Thy throne O GOD is forever and ever a sceptre of righteousness is the sceptre of thy kingdom.

9. Thou hast loved righteousness and hated iniquity therefore GOD even thy GOD hath anointed thee with oil of gladness above thy fellows .
10. And Thou LORD in the beginning hast laid the foundations of the earth and the heavens are the works of thine hands."
Basi tuchambue hii mistari hapa juu kwa kutumia darubini mstari wa 8 Baba anamuambia Mwana kuwa Ufalme wako ewe Mungu ni wa milele hata milele hapa tunaanza kupata picha mpya kuhusu Yesu Kristo cha kwanza ni kwamba Yeye ni Mfalme na cha pili Ufalme wake ni wa milele hata milele, Pili ni kuwa Yeye ni Mungu na anayemuita Mungu ni Mungu hapa ndipo kama hujakaa kwenye kiti nakushauri uketi taratibu na mstari huu uko wazi kabisa kwamba Mungu Baba anamuita Yesu Kristo Mungu.
Mstari wa 9 tunaona kwamba Yesu alipenda haki na kuchukia uovu kwahiyo Mungu Mungu wako amekutia mafuta ya shangwe kupita wenzio.
Mstari wa 10 sasa ndipo mambo yanaponoga na kumbuka kuwa nimekuambia uketi, katika mstari huu Mungu anamuita Yesu Kristo Bwana na kwamba hapo mwanzo Yeye yaani Yesu ndiye aliitia msingi ya nchi na mbingu ni kazi ya mikono yake najua sasa utaanza kukuna kichwa inakuaje lakini usiogope kwakuwa haya ni madogo tu lakini yatakuwa makubwa ukiendelea na mtazamo ambayo uliutumia wakati unasoma Injili ya Yohana.
Naelewa kuwa utakuwa bado huamini lakini hilo ndilo Neno la Mungu na hivyo inabidi uelewe kuwa dhambi ilivyoingia ilitutenga na Mungu hivyo basi Yeye Mungu akaacha enzi na kufanywa kuwa Mwana wa Adamu ili aje kutuunganisha wanadamu pamoja naye na hii ndio Injili au habari njema Yesu Kristo ni Mungu ni Mwana wa Adamu na tukikumbuka katika Genesis tunaona kuwa Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26-27) na dhambi ilivyoingia Adamu alivyopata mtoto huyu mtoto alichukua mfano wa baba yake Adamu ambaye ni mdhambi (Mwanzo 5:3) kwahiyo baada ya dhambi kuingia ule Utukufu ambao mwanadamu alikuwa nao uliondolewa na dhambi na hii ndio kazi ya Yesu aliyokuja kufanya Yeye alikuwa ni Mwana wa Adamu na Alikuja kuurudisha ule Utukufu ambao Adamu na Hawa waliupoteza baada ya kuanguka dhambini na wote wanaomkubali wanafanya kuwa wana wa Mungu yaani wanazaliwa upya wanaondolewa dhambi kwa maji yaani Ubatizo na wanapewa ule Utukufu ambao Adamu alikuwa nao yaani Roho Mtakatifu kwahiyo baada ya Adamu kushindwa kufanya kazi aliyopewa na Mungu basi Mungu mwenyewe anakuja ulimwenguni na kumkomboa mwanadamu na kumfanya awe mwana wa Mungu Aliye juu.
Sasa bila Yesu Kristo ondoleo la dhambi halipo ukombozi wa mwanadamu haupo na pia mwanadamu hatoweza kuwa pamoja na Mungu kama Adamu alivyokuwa akiongea na Mungu Eden na ndiyo maana hata Yesu mwenyewe anaelezea kuwa ni Upendo wa ajabu alionao kwa ajili ya mwanadamu aliyeasi na kuanguka katika dhambi kwa sababu aliacha enzi na kuja kumfia.
Mheshimiwa hii ndio Injili kwa ufupi kabisa na Biblia nzima ni Kitabu kinachoelezea jinsi ambavyo Mungu anahangaika kumkomboa mwanadamu aliyemuumba na akaanguka katika dhambi halafu baadae Yeye Mwenyewe anakuja kumkomboa huu ni Upendo wa Ajabu usioelezeka.
 
Ajabu Sana ,,Mungu alipo kufa ,Na viumbe vyake vikaendelea kuishi ,,,sitaamini uungu wa yesu mpaka na kufa
 
Kwa hiyo bibi unakubali pia Yesu hakufa bali alinyakuliwa na kwa mujibu wa Quran kila nafsi itaonja mauti vp hapo kwa Yesu
 
Huu utata wa Yesu ni Mungu au sio Mungu ni wazi kuwa biblia ina tatizo,kwa sababu hili si tatizo la kutofautiana uelewa tu wa kutafsiri maandiko bali maandiko yenyewe pia huchanganya watu.

Hivyo huu ubishi unatia mashaka usahihi wa biblia.
unaamini Quran haina tatizo nikuumbue hapa kuhusu kuchanganya hadithi za kucopy?
 
Aahhh, hii kali, c ungeongeza nyingine!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…