Msaada wa Imani

Msaada wa Imani

Ukishafahamu kuwa Allah sio Mungu anayezungumzwa kwenye biblia wala hutapata taabu ya kuumiza kichwa bali utajikita kufanya yale yanayoagizwa kwenye imani yako. Sidhani kama umeshamaliza yale yote uliyoagizwa na imani yako na kwamba upo safi kwa ajili ya maisha yajayo kwa mujibu wa imani yako.
Asante!
 
Ahh kumbe nimsubirie tu. Raha kweli.okay wacha nisubiri
Tena tulia kabisa kama alif.mpaka muda ukifika kila goti litapopigwa na kila ulimi utapokiri ndiyo utakuwa muda sahihi wa wewe kujua,sasa hivi utajilisha upepo tu.muda wako bado achia wanaojua.
 
Tena tulia kabisa kama alif.mpaka muda ukifika kila goti litapopigwa na kila ulimi utapokiri ndiyo utakuwa muda sahihi wa wewe kujua,sasa hivi utajilisha upepo tu.muda wako bado achia wanaojua.
Ohh kwahiyo ukijua huna wajibu wa kumfundisha ambae hajui. Mbona Dini ya kichoyo hii? [emoji45]
 
Hilo ni neno pekee ambalo MUNGU amekufungulia ufahamu wako, ukaweza kulitambua, kwanni hujiuliz nan alimtuma na kwa sababu gani alitumwa? Au unajifunza ku-quote?

Alitumwa na Allah kama walivyotumwa mitume wengine wote.

Hebu nionyeshe hicho nilicho "quote" hata ukaona nnajifunza. Ukishindwa kukionesha hapo ulipo ni quote ina maana huelewi maana ya neno QUOTE.
 
Sioni sababu ya kuanza kirudia yote niliyoyaandika. Hebu pitia post vizuri ndio utaelewa mjadala wetu.
Nimesoma kuanzia mada hadi post sijaona mahali ambapo nitapata nilichokuuliza,unaweza kunionesha?
Pili kuvaa kanzu sio desturi ya waarabu. Hata Yesu wako alivaa kanzu na kilemba [emoji23] [emoji23]
Kuvaa kanzu kunaweza kuwa ni mavazi ya zaidi ya Waarabu lakini dini ya Kiislam ndiyo inawataka waumini wake wavae kanzu na vazi hilo ni vazi linalotambulika kama vazi la dini hiyo.Huyo Yesu uliymtaja hapo aliwahi wapi kuwaagiza wanaofuata maelekezo yake wavae kanzu?
 
Kuna Mtu Alisema Yesu kaumbwa kabla ya Mwanadamu wa Kwanza. Ndio mie nikamjibu kwamba kumbe kaumbwa!! Nawe ukauliza Yesu gani kaumbwa?

anyways isiwe issue. We unahisi Yesu hakuumbwa? Je unafahamu kua Yesu ana Mungu wake? Je unafahamu Kuwa Yesu hajui kila kitu?
Unaniuliza kuhus Yesu gani?

Kwenye klabu ya Manchester Cuty kuna mchezaji anaiwa Yesu,nitaelewaje kuwa humsemi huyu?

Kwanini unapouliza usiulize swali lililokamilika kwa kusema ni nani mwenye sifa zipi unayemuulizia?
 
Hilo deni la dhambi Mungu ambae nimuweza wa kila Jambo hawezi kulisamehe mpaka atoe kafara ya kifo na damu kwa mwanae? Ninavyojua mimi Mungu hata leo akiamua kutusamehe dhambi zetu anatusamehe tu. Hiyo kafara ya mpaka amuue mwanae kweli inaingia akilini? Yaani wewe uibe na ufanye uzinzi halafu badala ya kukusamehe niamue kumuua mtoto wangu? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] duh huyu atakua Mungu wa kafara sasa !!

Mkuu Jaffar;
Kwana nashukuru uliisoma thread hii. Sasa nakuomba rudia tena mchango wangu. Naona umesha sahau nilosema. Aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, kwanza hawezi kufikiriwa kwa akili zetu.
Kuhusu kafara aliyoitoa, kwako wewe ni shida kidogo kuielewa ila naomba nikuambie hivi: Dhambi ni mauti. Thambi ni Kifo. Dhambi ikiisha kukuteka hukuondoa kabisa kwenye uwepo wa Mungu. Mungu, kwa makusudi yake mwenyewe, aliitoa nafsi yake ife msalabani ili kutulipia hilo deni la dhambi zetu. Huwezi kumokota mtu aliyedondoka bila wewe kuinama. Mungu akaumwaga uhai wake, ili sisi tuliokuwa tumekufa kwa dhambi zetu, tupate kuwa hai tena kwa kifo chake.
Unapomchukulia Yesu Kristo kama mtoto wa mtu fulani, hapo ndipo unapoteza umaana wake kuutwaa mwili. Naomba nikuambie hivi; Ni Mungu aliamua kuitoa nafsi yake ili akuokoe weye.
Mafundisho ni mengi siwezi kukujibu kwa hapa
 
Yeye ndie mwana wa Mungu,
Jaffar, unamaanisha huwez kufanya kazi aliyokutuma baba yako, ok unadhani unashindwa kusimama kama baba yako kwa mambo mbali mbali ya mzee wako?
Tukisema mwana wa Mungu unapata ufahamu upi? Hivi mtoto wa mbwa ni paka eti,au? Ufahamu na fikra ndio tatizo KUBWA. YESU hasingeweza kusurubiwa pamoja na nguvu ya kiungu, ndio maana alilia msalabani akimwambia mungu mbona umeniacha juu ya msalaba alikuwa binadam totally hadi kufa na kuzikwa , baada ya kufufuka alikuwa si mwanadamu tena japo nyie watoto wa mamdogo hamuamin hivo na si kwa IMAN ya kwel bali ya kupandikizwa
Mbwa akizaa mtoto mwenye sifa za paka kabisa kwa kila kitu,huyo mtoto hatuwezi kumwita mbwa kisa kazaliwa na mbwa bali tutamwita mtoto wa mbwa ila yeye ni paka.

Hivyo huyo mtoto atakuwa ni paka na si mbwa,kila kiumbe kina sifa zake.
 
Habari wana JF. naomba kufahamishwa kuhusu Yesu Mtoto wa Mariam. Je Imani ya Wasabato, Waroma na Madhehebu mengine wanamchukulia kama Nani? Je ni Mungu? Mwana wa Mungu ama Mtume wa Mungu? Asanteni.
Yesu ni Mungu...

Wasabato siyo Wakristo hivyo wanamchukulia Yesu kama Nabii sawa na Ellen G White...
 
Mkuu;
Unapotaka kumfikiri Mungu kinadharia inakuwa ngumu kuelewa. Neno moja fupi tu ni kuwa; Amini kwamba, Yesu ni Mungu. Yaani, baada ya mwanadam kuanguka, Mungu alitaka kumrudisha kwake. Aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Kumbuka; Hakuumbwa mwingine yeyote kwa mfano na sura ya Mungu kama mwanadam.
Hivyo, akatakiwa, mwanadam kweli, amkomboe (amlipie) deni mwanadam. Mungu akasema, awepo wa kufanana na mwanadam amkomboe mwanadam. Kwa sababu; Dam ya mnyama haikusaidia ikatakiwa dam isio na hatia. Mungu, akalituma neno lake, likafanyika mwili (mtu) akaishi ka sisi, akajaribiwa ka sisi lakini hakutenda dhambi. (Yesu).
Mkuu, ni furaha kuamini hivyo kwani aliyeumba mbingu na nchi huwezi kumfaham kwa ubongo wako weye kwani nao aliuumba. Chukulia tu hivi; Aliyeumba hawezi lingana na aliyeumbwa.
Yesu ni Mungu kamili na mtu kamili.
"Yesu ni Mungu kamili na binadamu kamili"

Hebu fafanua.
 
Sioni sababu ya kuanza kirudia yote niliyoyaandika. Hebu pitia post vizuri ndio utaelewa mjadala wetu.
Pili kuvaa kanzu sio desturi ya waarabu. Hata Yesu wako alivaa kanzu na kilemba [emoji23] [emoji23]
Mnamaanisha nini mnaposema YESU KRISTO...!!? Naona wengi humu wanakula matapishi yao...!! Maana mnajichanganya pasipo kujuana...!!

Huwezi kumtaja YESU bila kuweka KRISTO mbele yake.....hivyo elewa unapo sema MPINGA KRISTO...unamaanisha mpinga mafunzo/mafundisho ama maongozo ya Yesu...
 
Mnamaanisha nini mnaposema YESU KRISTO...!!? Naona wengi humu wanakula matapishi yao...!! Maana mnajichanganya pasipo kujuana...!!

Huwezi kumtaja YESU bila kuweka KRISTO mbele yake.....hivyo elewa unapo sema MPINGA KRISTO...unamaanisha mpinga mafunzo/mafundisho ama maongozo ya Yesu...

Tulioulizwa tunapaswa kujibu swali au kunyamaza na siyo kutukanana.Nitajibu kwa kadri ya uelewa wangu kwa mujibu wa Biblia.Madhehebu yote uliyoyataja ni sehemu ya Ukristo,si Ukristo.Kwa wakristo wote( wafuasi wa Yesu Kristo) huamini yafuatayo:-

Yesu ni MUNGU,ni mwana wa MUNGU, aliumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.Ni nuru,ni njia,kweli na uzima.
Atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.Kwake yeye kila ulimi utakiri na kila goti litapigwa.

Kwa aamininiye haya ana uhuru wa kuamua huyu ni nani.Lililo muhimu siyo kujua kama ni MUNGU,mwana wa MUNGU au nabii.Wanafunzi wake walimuuliza swali hili akiwa nao naye alilijibu kwa kuwauliza "Ninyi mwasema mimi ni nani?"

Kila amwaminiye hahukumiwi ,kila asiye mwamini amekwisha kuhukumiwa.
 
"Yesu ni Mungu kamili na binadamu kamili"

Hebu fafanua.

Mkuu;
Kama unaamini kuwa Yesu ni Mungu kamili basi usimtetee kwani Mungu hatetewi hujitetea mwenyewe. Uwezo huo anao kama ukimwomba ajidhihirishe kwako. Hapa huna haja ya kuwa na imani. No, mwombe tu kuwa ungeomba aidhihirishe kwako naye hufanya.
 
Mkuu;
Kama unaamini kuwa Yesu ni Mungu kamili basi usimtetee kwani Mungu hatetewi hujitetea mwenyewe. Uwezo huo anao kama ukimwomba ajidhihirishe kwako. Hapa huna haja ya kuwa na imani. No, mwombe tu kuwa ungeomba aidhihirishe kwako naye hufanya.
Sijakuelewa.
 
Quran tukufu inasema hivi,"Na kwa kauli yao kuwa: ‘Tumemuua Yesu mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu’. Hakika ni kuwa hawakumuua wala hawakumsulubu, lakini walishabihishiwa kwao. Wale wanaotofautiana katika hilo wako katika shaka wala hawana ilimu ya uhakika kuhusu hilo, wanafuata tu dhana. Hakika ni kuwa hawakumuua".
"Bali Mwenyezi Mungu Alimnyanyua Kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima". [An-Nisaa: 157-158]
 
Unaniuliza kuhus Yesu gani?

Kwenye klabu ya Manchester Cuty kuna mchezaji anaiwa Yesu,nitaelewaje kuwa humsemi huyu?

Kwanini unapouliza usiulize swali lililokamilika kwa kusema ni nani mwenye sifa zipi unayemuulizia?
Dont beat around the Bush my Friend. Unajua Exactly ni yupi tunamuongelea.
So please nipe majibu kama unayo.
 
Back
Top Bottom