Msaada wa Imani

Asante!
 
Ahh kumbe nimsubirie tu. Raha kweli.okay wacha nisubiri
Tena tulia kabisa kama alif.mpaka muda ukifika kila goti litapopigwa na kila ulimi utapokiri ndiyo utakuwa muda sahihi wa wewe kujua,sasa hivi utajilisha upepo tu.muda wako bado achia wanaojua.
 
Tena tulia kabisa kama alif.mpaka muda ukifika kila goti litapopigwa na kila ulimi utapokiri ndiyo utakuwa muda sahihi wa wewe kujua,sasa hivi utajilisha upepo tu.muda wako bado achia wanaojua.
Ohh kwahiyo ukijua huna wajibu wa kumfundisha ambae hajui. Mbona Dini ya kichoyo hii? [emoji45]
 
Hilo ni neno pekee ambalo MUNGU amekufungulia ufahamu wako, ukaweza kulitambua, kwanni hujiuliz nan alimtuma na kwa sababu gani alitumwa? Au unajifunza ku-quote?

Alitumwa na Allah kama walivyotumwa mitume wengine wote.

Hebu nionyeshe hicho nilicho "quote" hata ukaona nnajifunza. Ukishindwa kukionesha hapo ulipo ni quote ina maana huelewi maana ya neno QUOTE.
 
Sioni sababu ya kuanza kirudia yote niliyoyaandika. Hebu pitia post vizuri ndio utaelewa mjadala wetu.
Nimesoma kuanzia mada hadi post sijaona mahali ambapo nitapata nilichokuuliza,unaweza kunionesha?
Pili kuvaa kanzu sio desturi ya waarabu. Hata Yesu wako alivaa kanzu na kilemba [emoji23] [emoji23]
Kuvaa kanzu kunaweza kuwa ni mavazi ya zaidi ya Waarabu lakini dini ya Kiislam ndiyo inawataka waumini wake wavae kanzu na vazi hilo ni vazi linalotambulika kama vazi la dini hiyo.Huyo Yesu uliymtaja hapo aliwahi wapi kuwaagiza wanaofuata maelekezo yake wavae kanzu?
 
Unaniuliza kuhus Yesu gani?

Kwenye klabu ya Manchester Cuty kuna mchezaji anaiwa Yesu,nitaelewaje kuwa humsemi huyu?

Kwanini unapouliza usiulize swali lililokamilika kwa kusema ni nani mwenye sifa zipi unayemuulizia?
 

Mkuu Jaffar;
Kwana nashukuru uliisoma thread hii. Sasa nakuomba rudia tena mchango wangu. Naona umesha sahau nilosema. Aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, kwanza hawezi kufikiriwa kwa akili zetu.
Kuhusu kafara aliyoitoa, kwako wewe ni shida kidogo kuielewa ila naomba nikuambie hivi: Dhambi ni mauti. Thambi ni Kifo. Dhambi ikiisha kukuteka hukuondoa kabisa kwenye uwepo wa Mungu. Mungu, kwa makusudi yake mwenyewe, aliitoa nafsi yake ife msalabani ili kutulipia hilo deni la dhambi zetu. Huwezi kumokota mtu aliyedondoka bila wewe kuinama. Mungu akaumwaga uhai wake, ili sisi tuliokuwa tumekufa kwa dhambi zetu, tupate kuwa hai tena kwa kifo chake.
Unapomchukulia Yesu Kristo kama mtoto wa mtu fulani, hapo ndipo unapoteza umaana wake kuutwaa mwili. Naomba nikuambie hivi; Ni Mungu aliamua kuitoa nafsi yake ili akuokoe weye.
Mafundisho ni mengi siwezi kukujibu kwa hapa
 
Mbwa akizaa mtoto mwenye sifa za paka kabisa kwa kila kitu,huyo mtoto hatuwezi kumwita mbwa kisa kazaliwa na mbwa bali tutamwita mtoto wa mbwa ila yeye ni paka.

Hivyo huyo mtoto atakuwa ni paka na si mbwa,kila kiumbe kina sifa zake.
 
Habari wana JF. naomba kufahamishwa kuhusu Yesu Mtoto wa Mariam. Je Imani ya Wasabato, Waroma na Madhehebu mengine wanamchukulia kama Nani? Je ni Mungu? Mwana wa Mungu ama Mtume wa Mungu? Asanteni.
Yesu ni Mungu...

Wasabato siyo Wakristo hivyo wanamchukulia Yesu kama Nabii sawa na Ellen G White...
 
"Yesu ni Mungu kamili na binadamu kamili"

Hebu fafanua.
 
Sioni sababu ya kuanza kirudia yote niliyoyaandika. Hebu pitia post vizuri ndio utaelewa mjadala wetu.
Pili kuvaa kanzu sio desturi ya waarabu. Hata Yesu wako alivaa kanzu na kilemba [emoji23] [emoji23]
Mnamaanisha nini mnaposema YESU KRISTO...!!? Naona wengi humu wanakula matapishi yao...!! Maana mnajichanganya pasipo kujuana...!!

Huwezi kumtaja YESU bila kuweka KRISTO mbele yake.....hivyo elewa unapo sema MPINGA KRISTO...unamaanisha mpinga mafunzo/mafundisho ama maongozo ya Yesu...
 

Tulioulizwa tunapaswa kujibu swali au kunyamaza na siyo kutukanana.Nitajibu kwa kadri ya uelewa wangu kwa mujibu wa Biblia.Madhehebu yote uliyoyataja ni sehemu ya Ukristo,si Ukristo.Kwa wakristo wote( wafuasi wa Yesu Kristo) huamini yafuatayo:-

Yesu ni MUNGU,ni mwana wa MUNGU, aliumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.Ni nuru,ni njia,kweli na uzima.
Atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.Kwake yeye kila ulimi utakiri na kila goti litapigwa.

Kwa aamininiye haya ana uhuru wa kuamua huyu ni nani.Lililo muhimu siyo kujua kama ni MUNGU,mwana wa MUNGU au nabii.Wanafunzi wake walimuuliza swali hili akiwa nao naye alilijibu kwa kuwauliza "Ninyi mwasema mimi ni nani?"

Kila amwaminiye hahukumiwi ,kila asiye mwamini amekwisha kuhukumiwa.
 
"Yesu ni Mungu kamili na binadamu kamili"

Hebu fafanua.

Mkuu;
Kama unaamini kuwa Yesu ni Mungu kamili basi usimtetee kwani Mungu hatetewi hujitetea mwenyewe. Uwezo huo anao kama ukimwomba ajidhihirishe kwako. Hapa huna haja ya kuwa na imani. No, mwombe tu kuwa ungeomba aidhihirishe kwako naye hufanya.
 
Mkuu;
Kama unaamini kuwa Yesu ni Mungu kamili basi usimtetee kwani Mungu hatetewi hujitetea mwenyewe. Uwezo huo anao kama ukimwomba ajidhihirishe kwako. Hapa huna haja ya kuwa na imani. No, mwombe tu kuwa ungeomba aidhihirishe kwako naye hufanya.
Sijakuelewa.
 
Quran tukufu inasema hivi,"Na kwa kauli yao kuwa: ‘Tumemuua Yesu mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu’. Hakika ni kuwa hawakumuua wala hawakumsulubu, lakini walishabihishiwa kwao. Wale wanaotofautiana katika hilo wako katika shaka wala hawana ilimu ya uhakika kuhusu hilo, wanafuata tu dhana. Hakika ni kuwa hawakumuua".
"Bali Mwenyezi Mungu Alimnyanyua Kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima". [An-Nisaa: 157-158]
 
Unaniuliza kuhus Yesu gani?

Kwenye klabu ya Manchester Cuty kuna mchezaji anaiwa Yesu,nitaelewaje kuwa humsemi huyu?

Kwanini unapouliza usiulize swali lililokamilika kwa kusema ni nani mwenye sifa zipi unayemuulizia?
Dont beat around the Bush my Friend. Unajua Exactly ni yupi tunamuongelea.
So please nipe majibu kama unayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…