JaffarMohammed
JF-Expert Member
- Nov 13, 2016
- 762
- 283
- Thread starter
-
- #141
Hapo ndipo njia zinapopishana ndugu. Sisi waislamu tunaamini Mungu ni muweza wa kila Jambo. Ikiwemo la kukusamehe wewe Dhambi zako. Yaani kwa kifupi hana haja ya Kujibadili awe mwanadamu halafu Afe ndio yeye tena huyo huyo aliokufa atusamehe? Whats the point kufa then kufufuka? Ndio maana nikasema Mungu si Kama wachawi wa kutaka Kafara fulani ya Damu ya Mtu ili Jambo litimie!Mkuu Jaffar;
Kwana nashukuru uliisoma thread hii. Sasa nakuomba rudia tena mchango wangu. Naona umesha sahau nilosema. Aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, kwanza hawezi kufikiriwa kwa akili zetu.
Kuhusu kafara aliyoitoa, kwako wewe ni shida kidogo kuielewa ila naomba nikuambie hivi: Dhambi ni mauti. Thambi ni Kifo. Dhambi ikiisha kukuteka hukuondoa kabisa kwenye uwepo wa Mungu. Mungu, kwa makusudi yake mwenyewe, aliitoa nafsi yake ife msalabani ili kutulipia hilo deni la dhambi zetu. Huwezi kumokota mtu aliyedondoka bila wewe kuinama. Mungu akaumwaga uhai wake, ili sisi tuliokuwa tumekufa kwa dhambi zetu, tupate kuwa hai tena kwa kifo chake.
Unapomchukulia Yesu Kristo kama mtoto wa mtu fulani, hapo ndipo unapoteza umaana wake kuutwaa mwili. Naomba nikuambie hivi; Ni Mungu aliamua kuitoa nafsi yake ili akuokoe weye.
Mafundisho ni mengi siwezi kukujibu kwa hapa
Yaani kwa kifupi haiwezekani Mungu kushindwa kuWasamehe watu aliowaumba Yeye mwenyewe mpaka Amwage Damu ?
Anyways kwa uelewa wangu watu wengi wakienda kuungama Dhambi makanisani mchungaji anawaambia Nenda Umesamehewa! Je mchungaji ana nguvu kuliko Mungu?