Msaada wa jinsi ya kupata cheti cha kifo

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,149
Reaction score
3,963
Bila kupoteza mda nawasalimu nyote na pole na majukumu ya kujiingizia kipato.

Baada ya Baba yangu mzazi kupata ajali ya Gari Ghafla alikimbizwa kituo Cha Afya Kijijini kwetu na hatimaye juhudi za kuokoa maisha yake zikakwama na ndipo alikufa majira ya Saa 10 Jioni siku ya tarehe 07/12/2022.

Msaada ambao ninauomba kwenu Ni jinsi ninavyoweza kupata CHETI Cha KIFO Cha baba yangu. Napenda kujua:
  • Ni taratibu gani zinatakiwa kufuatwa?
  • Ni vitu gani vinahitajika?
  • Ni wapi pa kuanzia?
  • Inachukua muda gani?

Aksanteni Sana.

R.I.P to My beloved Father.
 
Nenda ofisi ya rita utapewa taratibu zote.
 
Nenda ofisi ya serikali ya mtaa wako au kata Yako. Mtendaji atakupa barua inayokutambulisha wewe kuwa ni mtoto wa marehemu na taarifa za marehemu.

Ukipata barua hiyo pia Kuna muhtasari wa kikao Cha familia unaokuruhusu kuchukua hicho cheti lengo ni kuepusha migogoro iwapo watoto ni wengi au wa wake tofauti.

Ukiwa navyo hivyo vyote (barua na muhtasari) fika Rita ukiwa na Hela chini ya elfu tano utakayoitoa Kama ghalama(zamani ilikua 3000)
 
Nashukuru Sana Ndugu yangu.
 
Napenda kuuliza kidogo.

Je,Huo mhitasari wa Kikao Cha Familia unatakiwa uweje? Au Uhusu Nini? Majina ya wanafamilia yanahutajika?
 
Napenda kuuliza kidogo.

Je,Huo mhitasari wa Kikao Cha Familia unatakiwa uweje? Au Uhusu Nini? Majina ya wanafamilia yanahutajika?
Muhtasari wowote majina ya wanafamilia, uhusiano wao na marehemu na sahihi zao vinahitajika. Taarifa hizo zitakuwepo kwenye karatasi la mahudhurio.

Muhtasari unakua ni kama taarifa fupi ya wanafamilia. Tafuta mtu anaeweza kuandaa muhtasari akusaidie kuuandaa. Ukikwama Sana tuwasiliane nikupe muongozo uandae mwenyewe.
 
Pole na Msiba, Baba alifia wapi hospitali gani? Na je una kibali cha mazishi? Na kwenye kibali hicho cha mazishi limeandikwa jina la nani alipokea mwili?
Ukinijibu hivi nitakupa maelezo mazuri na jinsi ya kupata kwa muda mfupi…
 
Ndo siku nane tu zimepita, mkuu unatafuta cheti cha kifo hata huzuni imekuisha lini? Mmi siwezi kuwa na ujasiri huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…