Msaada wa kiafya

Msaada wa kiafya

Wings

Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
70
Reaction score
11
Wanajf naombeni msaada kwa tatizo linalonisibu, kila ninapotoka kuoga ndani ya dakika chache ngozi yangu huwa inawasha sana. Nimejaribu kutumia medicated soap lakini bado tatizo liko palepale. Maji nayo sidhani kama ni issue kwani sehemu yoyote ninapokua nimekwenda hali ni hiyo hiyo. Ndugu zangu nisaidieni.
 
Wanajf naombeni msaada kwa tatizo linalonisibu, kila ninapotoka kuoga ndani ya dakika chache ngozi yangu huwa inawasha sana. Nimejaribu kutumia medicated soap lakini bado tatizo liko palepale. Maji nayo sidhani kama ni issue kwani sehemu yoyote ninapokua nimekwenda hali ni hiyo hiyo. Ndugu zangu nisaidieni.


tatizo lako lina muda gani??
 
Maji,nguo ya kujifutia,unayovaa zote zaweza kuleta hiyo tatizo.....sehemu yeyote unapokwenda ni wapi?inaweza ikawa kuzunguka eneo unalohishi lote mnatumia maji ya chanzo kimoja.chunguza hilo.....
 
Ni zaidi ya miaka minne sasa.

Miaka nne mingi sana mkuu. umejaribu kumuona daktari na kumuelezea tatizo lako? Umejaribu kuchemsha maji na kuona kama kuna tofauti?

Mwagia Detol kwenye hayo maji hili ucheki kama bado kama utakuwa unawashwa tu na je nguo zako unaanika wapi au taulo lako unalifua kila baada mda gani vitu kama hivyo muhimu pia kuangalia.
 
Inawezekana ni tatizo la ngozi kuwa kavu. Kama unawashwa kwa muda tu, ni ukavu wa ngozi yaani inakuwa inavuta. So mara umalizapo kuoga paka lotion. Mimi si doctor lakini nimeshawahi feel same nilipokuwa nchi fulani wakati wa winter. Jaribu kupaka lotion.
 
Kama bado haujatatua tatizo lako, nakusahuri uende Tumaini Hospital Upanga au wapigie kwa +255773659153 kufanya booking ya kuonana na bingwa wa magonjwa ya ngozi (Dermatologist)
 
Hujatwambia kama kuna mabadiliko kwenye ngozi yako...kama hakuna mabadiliko yoyote , tatizo lako linaweza likawa kichwani tu...(somatization)..unahitaji psychotherapy mtafute psychologist.
 
Pole sana. Onana na madaktari wa ngozi watakusaidia.
Unawashwa baada ya kujifuta maji au kabla?
Kama baada inawezekana una aleji na material ya taulo.
 
Back
Top Bottom