Msaada wa kidaktari, nahisi nimepata Gonorea

Msaada wa kidaktari, nahisi nimepata Gonorea

Mbuna Senior

Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
55
Reaction score
125
Habari za leo wana jamvi,

Naomba msaada wa kitabibu nimepata ugonjwa wa zinaa nahisi ni gono maana usaa unatoka kwa wingi na pia nasikia maumivu makali wakati wa kujisaidia haja ndogo.

Nimepata ushauri na marafiki maana nimeona aibu kwenda hospital nikanunua dawa za fragil, doxy na cipro nimetumia hadi dozi imeisha ila bado hali ya kutoka usaa inaendelea ingawa maumivu yamepungua pia ninajitahidi kunywa maji mengi na mkojo unatoka mweupe kama kawaida ila nikiamka asubuhi naona usaa unegandia.

Naomba ushauri maana naumia kisaikolojia. Ahsanteni
 
Ooooh mama yangu, kama unajipenda nenda hospital unless utakosa tena fursa ya kufanya hilo tendo kwa maisha yaliyobaki. Plz wala usione aibu kbs, nenda na utapata matibabu ya uhakika.
 
Ugonjwa hauna aibu ndugu yangu
Wahi kituo cha Afya mapemaa
Jali afya yako usijali watu watasema nini ama watakuonajee
Pole sana ndugu
 
Back
Top Bottom