Msaada wa kielimu kwa mdogo wetu wa kike

Mpeleke VETA akasome course ya chaguo lake kwa manufaa yake ya baadae.
 
Muulizeni mwenyewe anataka nini kuliko kumpeleka kule mnapotaka nyinyi.

Unaweza kuta mwenyewe anapenda kupika, sasa kuliko kumpeleka nursing mpelekeni akasomee mapishi.

Kuna mpwa wangu wa kike alikuwa mtu wa kuzungusha zero maisha yake yote ya shule.
Alipomaliza Form 4 na matokeo kutoka na zero baba yake akataka kumpeleka Uganda A level. Binti alikuwa analia tu kuwa hataki kusoma.

Nilipomuuliza vizuri anataka nini, akasema yeye anapenda mambo ya urembo yani kupamba watu.
Niliwaambia wazazi wake, baba yake akawa mkali sana na kukataa kumsomesha.

Nilichukua jukumu la kumpeleka Beauty Course ya miezi 6.
Akiwa anaendelea baada ya miezi 3 mwenye chuo (ni mama wa kihindi) alivutiwa nae sana kiasi cha kuamua kumsomesha bure kwa sharti la kuwa msaidizi wake pale atakapomaliza.

Hii ilikuwa ni 2021, mpaka leo hii yule binti kafungua beauty parlor yake mwenyewe, ambayo ina wateja wa corporate aliowapata kwa reference ya mwalimu wake ambae kwa sasa huyo mwalimu kahamia Dubai.
Maisha ya binti yanakwenda vizuri bila utegemezi wa mtu yeyote yule.

Kuna stage ikifika inapaswa tuulize nini watoto wanataka na sio kulazimisha matakwa yetu kwao.
 
hii haina kufeli labda asiandike kitu aache blank
 
Hukutoa msaada mkuu kama wewe na daktari mshahara unalipwa. Kama ni afisa kata,maendeleo etc hufanyi hio kazi bure.

Msaada hauna malipo
Ungejua nimeokoa wangapi kwenye hiyo jamiii usingesema hata hivyo
 
Hukutoa msaada mkuu kama wewe na daktari mshara unalipwa. Kama ni afisa kata,maendeleo etc hufanyi hio kazi bure.

Msaada hauna malipo
Mimi sio mfanyakazi serikalini wala Taasisi binafsi .
Mimi ni mwanafunzi wa UDSM ,Mpambanaji niliyeamua kujitoa kwaajili ya jamii zetu kuendelea nasio kuja kusema ni uvivu wao.
UNAONAJE UKAZUNGUKWA NA WATU AMBAO WOTE MNAMAFANIKIO ?
SASA MIMI NAONA NI BOLA KUONDOA UJINGA KWA HARI NA MALI.
 
Udsm unaandika BOLA badala ya BORA. HARI badala ya HALI

Duh aiseee
 
Udsm unaandika BOLA badala ya BORA. HARI badala ya HALI

Duh aiseee
Sidhani kama haya mambo uloona nimeyakosea yakirekebishwa yataongeza chochote kwenye pato la TAIFA.
Ebu kosoeni vyenye maana nasio hizi vitu waachieni wanafunzi wa sekondari bwana .
Au wewe unaona hili la maaana tuliongelee??πŸ€“
 
Arudie shule. Mtu unapataje 4 ya 31 huko shule hawafindishi au
 
Kitu kidogo tu kinaweza kukuangusha ukute kilichomuangusha dogo ni suala la muandiko akidhani wasahihishaji wataelewa tu
Sidhani kama haya mambo uloona nimeyakosea yakirekebishwa yataongeza chochote kwenye pato la TAIFA.
Ebu kosoeni vyenye maana nasio hizi vitu waachieni wanafunzi wa sekondari bwana .
Au wewe unaona hili la maaana tuliongelee??πŸ€“
 
Mtoa mada wewe kama wewe unamaono gani ukiweka mbali ulalamishi.

Wewe kama kaka au dada umempa ushauri gani.Kwa umri wako ni dhahiri unajua maisha yanataka nini hapa mavumbini Tz,so kwa kukusaidia wewe weka mawazo yako hapa tukushauri vizuri.
Komasavaa
 
Best option ni kureseat masomo matatu apate credits za kwenda chuo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…