Msaada wa kimahakama hapa ukoje

Msaada wa kimahakama hapa ukoje

RALO

Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
46
Reaction score
13
Kuna familia ya baba,mama na watoto watatu wa kiume,kati ya wale watoto watatu wawili ni wa nje ya ndoa mmoja kwa baba na mwingine kwa mama,mmoja ndiye aliyezaliwa ndani ya ndoa ila wote walikuwa wanalelewa kwenye nyumba moja....sasa ishu iko hivi:

Kwa bahati mbaya wazazi wote walifariki kwa nyakati tofauti na kila mmoja wa wale watoto alipewa sehemu ya urithi wake (nyumba na kiwanja) na wazazi wao baada ya kufariki,sasa baada ya muda mtoto wa mwisho kati ya wale watatu akafariki ambaye ndiye alikiwa ndani ya ndoa na hakuacha wosia wowote kuhusu mali yake ichukuliwe na nani maana na yeye alikuwa bado mwanafunzi,sasa ndugu nao wameingilia kati wanataka kugawana hizo mali,lakini kaka zake wa nje ya ndoa wapo hai.
Sasa kisheria huo mgawanyo wa mali unatakiwa uende kwa nani kihaki?
thanks in advance.
 
Siku hizi mtoto wa nje ya ndoa...ana haki sawa na watoyo waliozaliwa nje ya ndoa kama ni hivyo hao watoto wa nje ya ndoa wanahaki na hivyo vitu, lakini haki hio inatoka katika zile mali za wazazi wao awali..
 
sawa mkuu na unaposema mali za wazazi wao awali unamaanisha hzo alizorithi marehemu kutoka kwa wazazi tu?
 
sawa mkuu na unaposema mali za wazazi wao awali unamaanisha hzo alizorithi marehemu kutoka kwa wazazi tu?

Namaanisha mali za wazazi wao wote..hao..halafu kwa ufahamu wangu mimi mtu akifariki bila kuacha wosia, kama hana wazazi mali zitaenda kwa ndugu wa karibu ambapo hapo nahisi ni hao ndugu zake wa nje ya ndoa hasa hasa huyo aliezaliwa na baba yake maana ni ndugu wa karibu wasingekuwepo hao ingeenda kwa akina baba wakubwa au wengine hapo sijachambua vifungu...vya sheria...
 
Ok mkuu asante sana ...hapo nimekupata vilivyo
 
Back
Top Bottom