Msaada wa kimawazo: Nahisi naanza kupata depression

Msaada wa kimawazo: Nahisi naanza kupata depression

Hakuna dhambi mbaya kama kumuoa mwanamke kisa tu umezaa nae. Mahusiano hayo huambatana na majuto na mateso. Oa mtu kwasababu unampenda, una hisia nae na ukimuona tu unahisi kumfurahia
 
Kuna mambo mawili nitakushauri.
1. Wewe ndio utaishi naye. Kwa hio usifanye uamuzi mzito huu kwa kishinikizwa na Yeyote. Fuata moyo wako. Na kama moyo wako unasema hapana, basi Simama imara hapo. Sio wazazi wako, au wazazi wake, au yeye akushinikize. Maamuzi kama hayo ukifuata moyo wako. hautajuta hata siku moja.
2. Mchukue tu kama mke. Japo moyo haujaridhika. Ila mwanzishie mradi auendeleze. Na hapo ujue utachepuka sana sababu roho haijatulia kwa huyo. Itabidi akuvumilie tu kwa hilo.
Hapa kuna kitu kaka. Ushauri wako ntaufanyia kazi
 
Mkuu, jibu ni: Sio lazima. Na Sio lazima sasa hivi.

Kwanza aliyekwambia akizaa ndio hapo hapo unaoa ni nani?

Huhitaji kufanya maamuzi sasa hivi. Lea mwanao, mjali mama yake.

Mwisho wa siku kama mapenzi yapo yapo na kama hayapo hayapo tu. Hata yeye mwnyw atajua tu fungu sio lake. Kwa sasa usiwe na presha.

Watu wameoa wazazi wenzao after years wakati mtoto kashakuwa, wewe mtoto kazaliwa juzi tu unawaza ndoa?

Japo binafsi natamani ungemuoa huyo binti. Ila ushauri wangu ndio kama hapo juu. Sio lazima. Na sio lazima sasa hvi.
Kweli mkuu
 
Kutokuao ndio kukimbia majukumu.
Hajisikii kuoa, mnataka kumlazimisha.
Miaka 27 anakimbilia wapi?

Kuoa ni mzigo.

#YNWA
Mkuu mbona umekomaa na umri wa miaka 27? Huyu ni mtu mzima Unataka aje aoe na miaka mingapi
 
Depression ya nini? Wakati unafanya mpenzi bila kondom ulitegemea nini kijana?

Acha kukimbia majukumu, na uache kuchezea mabinti bila sababu za msingi, kaa uoe, maana utaishia kutengeneza idadi kubwa ya watoto wa nje bila sababu.

Acha woga ndoa tamu sana!
Hapo mwisho ndio ulipoharibu
 
Humpendi kwa sababu anakupenda Sana...

Endelea kuzingua utampata unayempenda kuliko anavyokupenda, ndo utajua anayopitia huyo mdada.

USHAURI WANGU: Kama huna sababu nyingine, mpende kwa sababu amekupenda.

Zaidi ya hapo, utajuta.
 
[emoji16][emoji16] Huyo Ni mbu aliye tua kwenye mbupu ukijifanya kumtoa kwa kumpiga Kofi tu imekula kwako
 
Alhamdullilah
Nilidhani mtoto si wako

hongera kuwa baba
Kuna mipango yako na kuna yale Mungu aliyokupangia...

muoe huyo binti inaonekana alikua mwaminifu kwako
Na mwanamke ambae ni waruwaru hawezi enda kwa Wakwe na confidence hiyo..she is a good woman
 
Eti Depression Ni ugonjwa was wazungu...Wewe utakuwa schizophrenia
 
Ndoa nyingi siyo plan ya muolewaji au muowaji.Zingine zinazuka tuu na maisha yanaendelea. Hayo maisha ya kuplan wewe siyo Mungu. Ndoa hiyo owa huyo binti
 
Chukua huyo ishi nae lea mtoto wenu. Unless kama unaweza kuvumilia mwanao kulelewa na mwanaume mwingine.
 
Ndoa raha ila kwa umpendae.
Binafsi ilinitokea 2015 niligoma kabisa.
Na kwasasa kila mtu ana maisha yake.

Kaolewa ila mimi kuoa bado sanaa 31 kwangu sio umri wa kuoa huu.

Maswala ya muoe tu eti kisa nimemzalisha "alitumwa kunitegeshea?"

Mtoto nitalea vizuri tu ila mama ake "Kila mtu ale hamsini zake"

Mapenzi hayalazimishwi, huja automatically.

#YNWA
We subiri uoe kwanza ndio utoe ushauri kwenye mada kama hizi. Acha wenye experience na ndoa watoe ushauri. Naona umevalia njuga asioe asioe, unajua uchungu wa mtoto alielelewa na mzazi mmoja wewe? Man up.
 
Ndugu yangu mleta uzi nakaribia kufanana nawe kimazingira yaliyonitokea.
Nikiwa na miaka 27 kama wewe nilioa mwanamke ambaye tayari nilikuwa na mtoto nae ingawa nami kwa kipindi hicho nilikuwa na ndoto nyingi sana na suala la kuoa lilikuwa mbali kabisa na fikra zangu.
Ila mimi niliamua 'kusacrifice' baadhi ya ndoto zangu kwa ajili ya ustawi wa mwanangu na mapenzi ya mwanamke wangu.
Leo hivi baada ya miaka 15 nami nikiwa baba wa watoto wanne maisha yanaendela na mapenzi yanazidi kustawi ndani ya ndoa yetu.
Wakati mwengine maisha ya ndoa na hatima ya tutakaokuja kuishi nao yanakuwa nje ya umiliki wetu.
 
We subiri uoe kwanza ndio utoe ushauri kwenye mada kama hizi. Acha wenye experience na ndoa watoe ushauri. Naona umevalia njuga asioe asioe, unajua uchungu wa mtoto alielelewa na mzazi mmoja wewe? Man up.
Yap Nina watoto wawili mmoja miaka 5 na mwengine 3 na wotee nawalea vizuri tu.

#YNWA
 
Yap Nina watoto wawili mmoja miaka 5 na mwengine 3 na wotee nawalea vizuri tu.

#YNWA
Sasa wewe hufai kumshauri huyu mtoa mada ushafeli, tena ukute hapo kila mtoto na mama yake. Unadhani utakuwa na familia ya namna gani? Sahau familia bora hapo.
 
Back
Top Bottom