Msaada wa kimawazo unahitajika

Msaada wa kimawazo unahitajika

Chalii flani

Member
Joined
Nov 5, 2021
Posts
67
Reaction score
166
Wajuba poleni na majukumu ya kuendelea kulijenga taifa letu wengi wetu tunapitia changamoto za kukatika umeme,maji na baadhi ya bidhaa kupanda wenye mamlaka huu mzigo tumewatwisha ninyi

Nije kwenye mada mjuba mwenzenu Kati ya ndoto zangu kubwa nilizowahi kuwa nazo tangu nakua ni kuja kumiliki gari la kutembelea katika njaro zangu za kila iitwapo Leo nimekua nikijiwekea visenti vidogo vidogo kwa takribani miaka name sasa Mungu hamtupi mja wake nimetenda chungulia kwenye akaunti majuzi nimekuta Kuna milioni 15

Kipekee naupenda Sana magari ya juu nikimaanisha aina ya rava 4,Forester new model,vanguard,x trail n.k ilimradi lisiwe chini Kama kina crown na nyingine aina hiyo

Msaada ninaohitaji kwanza Bei za magari sizijui naomba kufahamishwa kwa hiyo hela niliyokua nayo naweza kupata gari gani Kati ya hizo pendwa nilizotajwa hapo juu au Kama Kuna aina nyingine ya magari ya juu yatayoendana na kiasi nilichoko nacho

Natanguliza shukrani kwa wote mtakaonishauri asanteni
 
Back
Top Bottom