Msaada wa kimawazo

real hustler

Senior Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
143
Reaction score
204
Habari yako mwana jf

Baba yangu alibahatika kuwa na mali nyingi sana na kwetu tumezaliwa wachache watu wa nne tu,

Sasa mzee ili kuondoka utata ameamua kugawa mali ingali yupo hai Mimi nimepata mgao wa nyumba ya kuishi pamoja na kiasi kama million 50

Kwa upane wa elimu nina degree ya agribusiness kutokea SUA
Pia binafsi sina background yoyote ya kufanya biashara maana mda mwingi nimetumia shuleni

Niliwaza hii pesa niiweke UTT baada ya kuisoma na kuifatilia Sana lakini changamoto inakuja nahofia usalama wa pesa yangu huko UTT hasa hasa kwenye nchi yetu hii ambayo kiongozi anaweza amua chochote mda wowote.

Naombeni ushauri je naweza anzia wapi katika uwekezaji.
Na je UTT ni salama mathalani kwa miaka 30 ijayo. Umri wangu ni miaka 25.

Pia ningeomba Kwa wenye kujua zaidi ni mkoa gani au eneo gani Tanzania ni zuri Kwa mtu mwenye mtaji kuanza biashara na biashara ipi inaweza kuwa na rejesho zuri.
Asanteni


 
Wek
Weka tu
 
Usirogwe utt it's better uweke fixed account kama 40mil then 10mil nenda tabora miezi ya kwanzia mwez wa 3 mpka 5 ununue tumbaku ikiwa tayr imekaushwa ipo kwenye vishada nunua kwa kupoint then uiuze kwenye masoko mda wa masoko ukifika ni uhakika haina ugai gai unapiga pesa zako unatulia
 
Nyumba ipo eneo lipi? Strategic Area?

Sasa angalia condition ya nyumba ikiwezekana ifanyie REHABILITATION then ipangishe. Kama mwanzo ilikuw unapata 300k kwa mwezi ukifanya REHABILITATION ya 20m una uwezo wa kupata 600k.

Kitu ambacho kwa UTT huwez pata hiyo hela (300k) per mwezi.
 
Hii biashara ipo siku nitaifanya.
 
Kwa nini UTT sio nzuri Kwa maono yako ili niweze pembua mawazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ