Msaada wa kipimo mbadala

Msaada wa kipimo mbadala

Chagaboy93

Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
14
Reaction score
8
Wakuu habarini za wakati huu.

Nimeenda Muhimbili wameniandikia kipimo cha OGD. Kwa ninavyosikia hiki kipimo maumivu yake ni hatari. Naombeni msaada kama huwa kuna mbadala wake. Shida yangu kubwa ni maumivu ya kifua ya muda mrefu ila pia nimegundulika kuwa na vidonda vya tumbo.

Nilipewa dozi ikaisha ila hali bado iko palepale. Bad enough nimekuja kupata pia tatizo la koo kuuma kwa zaidi ya wiki tatu nikimeza kitu napata maumivu.Hali hii inanipa waswas mkubwa.
 
Kwanini usiende kwenye vipimo zaidi? Yaweza ikawa cancer!!,Kuna wakati Muhimbili ukiwa huna hela hata vipimo wanakupa batili ili uwaondelee kero tu mbele yao! Yawezekana si vidonda vya tumbo kama walivyokwambia!,siunamkubuka yule hawa aliyeimba na Diamondplatnumz ule wimbo wa NITAREJEA?

Yeye alienda kupima wakamwambia Ini limeharibika na linapelekea kuvimba tumbo, kumbe walimfanyia makusudi tu! Baada ya watu kumwomba Diamondplatnumz kumsaidia akampeleka India ikagundulika Moyo ndiyo ulikuwa na tatizo ,alifanyia oparesheni na hivi sasa anaendelea na maisha yake!.

Angeendelea kukomaa hapo muhimbili alikuwa anapoteza maisha,hiyo hospitali kuna tatizo kubwa mno na sijui ni nani atakuja kuwabadilisha hao wataalamu wetu,mishahara wanalipwa lakini hawatosheki.

Hilo tatizo lako usipochukua hatua zaidi ya vipimo utajikuta tatizo linakuwa kubwa,nenda hata ocean road ukapime uzizembee!!
 
Oesophago-gastro-duodenoscopy (OGD) au Gastroscopy (Endoscopy).

Fanya tu mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom