Kabala ya kugusia nini chanzo za tabia tulizo nazo ningependa nitoe maana fupi ya tabia: Tabia ni jumla ya matendo yote ayafanyayo mtu ama mnyama. Mambo haya yanajumuisha yale tunayoyaona kwa macho (mfano kula, kulala, kunywa, kutembea, kukonyeza, kuua, kuiba, kupigana, kusoma, nk) na yale tusiyoyaona kwa macho, mfano kufikiri, hisia zetu nk. Mambo makubwa mawili yanayofanya tuwe na tabia tulizo nazo
1. Urithi kutoka kwa wazazi wetu kibailojia.
2. Mazingira. Unapozungumzia mazingira unaangalia mambo mengi, mfano, watu wanaotuzunguka. Mtu anaweza akaiga tabia za mtu mwingine, misukumo (pressure) kutoka kwa watu wangu, malezi, ugumu wa mazingira tunamoishi, kiwango cha elimu nk. Kwa ujumla mazingira ni mambo yote ambayo sio ya kibaiolojia.
Hope imekupa mwanga.