Msaada wa Kisheria - Ajira tata

Marumeso

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2009
Posts
1,410
Reaction score
1,325
Kuna ndugu yangu aliitwa kufanya usaili katika shirika moja binafsi. Aliomba kazi baada ya kuona matangazo gazetini. Baada ya muda alipigiwa simu na kujulishwa amefaulu zoezi la usaili, hivyo anatakiwa aripoti kazini mara moja.

Siku ya kuripoti ilipofika, aliripoti katika ofisi husika akijua anaenda kukamilisha taratibu za ajira kama ilivyoelezwa kwenye simu. Lakini katika hali ya mshangao akakuta kuna mazingira ya kufanyika usaili mwingine!! Zamu yake ilipofika, aliingia na kuhojiwa maswali machache kisha akaambiwa arudi nyumbani atapigiwa simu.

Baada ya hapo ndugu yangu hajasikia lolote na sasa ni takribani mwezi wa 3-4, na kuna taarifa kuwa shirika limeshaajiri watu wengine nje ya walioitwa kwenye usaili.

Je naomba ushauri wa nini cha kufanya katika mazingira hayo niliyoyaeleza?
 
Ana ushahidi kama kweli walioajiriwa hawakuwepo kwenye usaili?
 
usaili ulikuwa ni WAZI na watahiniwa hawakuwa wengi kiasi msitambuane
Lets say watahiniwa walikuwa 10, kwahiyo unataka kuniambia wote 10 wameshawasiliana na hakuna hata mmoja aliesema yeye ndo aliepata hiyo kazi?
 
Lets say watahiniwa walikuwa 10, kwahiyo unataka kuniambia wote 10 wameshawasiliana na hakuna hata mmoja aliesema yeye ndo aliepata hiyo kazi?


Hawakufika hata hao 10.
 
Fanyeni ishu nyingine hapo hamna namna ya kumsaidia mAana hakuingia hata huo mkataba wala verbal agreement ya mkataba wa kazi...
 
Pia inawezekana wote mliokutana kwenye interview mlipigwa chini wakafanya mchakato upya na wakapata mtu mwingine. Sioni grounds za kumshtaki mwajiri maana kuitwa kwenye usaili sio guarantee ya ajira. Unaweza ukawa interbiew watu na usipate unayemtaka na hivyo kuamua kuanza zoezi upya. Alichokifanya mwajiri ambacho kidogo sio ustaarabu ni kutokuwapatia mrejesho waliosailiwa ili wajue nini kilitokea
 
Muuliza swali ana point.

Hapo kuna maswali mengi utajiuliza km ww ndo unakutana na hali km hiyo.

1.Kwa nini jamaa walimpigia cm kafaulu interview
2.Kwann wanampa 'interview' nyingine wkt walimwambia kafaulu aje kuanza kaz
3.Kwann unapita muda mrefu bila feedback
4.Kwann mtu mwingine asiyekuwepo kabisa kwenye interview anapata kaz kilaini
 
Kuna watahiniwa na watahiriwa..by the late Prof. Chachage..RIP..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…