Marumeso
JF-Expert Member
- Oct 3, 2009
- 1,410
- 1,325
Kuna ndugu yangu aliitwa kufanya usaili katika shirika moja binafsi. Aliomba kazi baada ya kuona matangazo gazetini. Baada ya muda alipigiwa simu na kujulishwa amefaulu zoezi la usaili, hivyo anatakiwa aripoti kazini mara moja.
Siku ya kuripoti ilipofika, aliripoti katika ofisi husika akijua anaenda kukamilisha taratibu za ajira kama ilivyoelezwa kwenye simu. Lakini katika hali ya mshangao akakuta kuna mazingira ya kufanyika usaili mwingine!! Zamu yake ilipofika, aliingia na kuhojiwa maswali machache kisha akaambiwa arudi nyumbani atapigiwa simu.
Baada ya hapo ndugu yangu hajasikia lolote na sasa ni takribani mwezi wa 3-4, na kuna taarifa kuwa shirika limeshaajiri watu wengine nje ya walioitwa kwenye usaili.
Je naomba ushauri wa nini cha kufanya katika mazingira hayo niliyoyaeleza?