Msaada wa kisheria (Criminal case)

Msaada wa kisheria (Criminal case)

Benaire

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2011
Posts
1,962
Reaction score
311
Kuna mtu mmoja alifoji saini ya bosi wake ili aweze kujipatia fedha.
Taasisi hiyo ikachukua hatua ya kumfukuza kazi....lakini nimesikia kuwa wamemfungulia mashtaka kwa kosa hilo hilo.
Je hapa kisheria imekaaje hii....naomba msaada wenu wajuvi wa sheria.
 
Duh hili jukwaa limeanza kupoa sana.....ule moto wa kisheria by Great Thinkers umenza ku-subside.
 
maelezo yako hayana nyama za kutosha, ngumu watu kukushauri maswala ya kisheria kwa maelezo finyu kama hayo
 
Thanks kwa ushauri.
Ni hivi huyo mtu ameshachukuliwa hatua ya kufukuzwa kazi...lakini bado kampuni inamshitaki mahakamani kwa kosa hilo hilo ambalo tayari wameshamhukumu!
Ndio nilitaka kujua je ni sahihi?
 
Kwa ufupi ni sahihi kutokana na maelezo yako mafupi, kufukuzwa kazi sio adhabu ya wizi pekee, kama sheria za kampuni zinasema kwa case za criminal mojawapo ya adhabu ni kufukuzwa kazi na kustakiwa basi kampuni ina haki ya kumshtaki
 
Kwa mawazo yangu mafupi....nilidhani ni vyema kampuni isingemfukuza bali kumsimamisha kazi na kumshtaki....kama mahakama ikimkuta na hatia ndio afukuzwe kazi...kwa kuwa mahakama ndio chombo pekee chenye kutoa hukumu ya hatia....suppose akashinda kesi mahakamani na walishamhukumu kwa kosa ambalo mahakama imeona sio kosa!
 
KAka kushinda Kesi mahakamani haimaanishi hauna kosa, unaweza ukawa na kosa lakini ushahidi ukawa haukizi vigezo vya kimahakama, hiyo ni tofauti na mambo ya kazi,

mfano kama wewe kwenye kazi hauko finance Department, na hauruhusiwi kuwa na chochote usichostahiri kuwa nacho kutoka Finance, sasa ukaja kuonekana una cheque ya Kampuni na hauna maelezo ya kutosha, au umeleta risiti za uongo, sasa kutokana na sheria ya Kampuni unaweza kufukuzwa kazi kwa kuhodhi vitu vya kampuni visivyokustahili au kwa kuleta risiti za uongo, lakini unaweza kwenda Mahakamani na huo ushahidi wa kampuni ukawa hauna nguvu,

hivyo mahakamani unaweza kushinda, lakini kwa vigezo vya kampuni ukawa una hatia
 
Thanks kwa kunielimisha.
Unajua kuna wakati tunaogopa kuingia hasara kwa mambo kama haya....nilidhani akishinda na wakati kahukumiwa kwa kosa hilo....anaweza kuishtaki kampuni kwa kumfukuza kwa criminal offense ambayo imekuwa null and void mbele ya mahakama.
 
kama kanuni za kampuni zinasema kwamba mojawapo ya makosa yanayopelekea summary dismissal ni a criminal offence wnaweza kukufukuza na baadae kukushtaki, lakini kwa faida yako baada ya mahakama kukuondoa hatia then unaweza fungua shauri CMA kwa ground ya unfair termination ukaomba kuwa compensated kutokana na kuwa terminated unfairly....
 
Kuna mtu mmoja alifoji saini ya bosi wake ili aweze kujipatia fedha.
Taasisi hiyo ikachukua hatua ya kumfukuza kazi....lakini nimesikia kuwa wamemfungulia mashtaka kwa kosa hilo hilo.
Je hapa kisheria imekaaje hii....naomba msaada wenu wajuvi wa sheria.
Sheria inasema hivi

(5) No displinary action in form of penalty, termination or dismissal shall lie upon an employee who has been charged with a criminal offence which is substantially the same until final determination by the Court and any appeal thereto.

Kwa maoni yangu naona kwa namna sheria ilivyokaa inaweza kuleta utata kiasi hasa katika suala lako. Kwa tafsiri yangu (Mie sio mwanasheria), naona hiyo sheria hapo inazuia mtu asipewe adhabu ya kinidhamu kama ameshafunguliwa mashitaka ya jinai kuhusiana na suala hilo hilo au linaloendana na hilo kwa kiasi kikubwa mapaka maamuzi ya mahakama yakishafanyika. Sheria naona haikuzuia Jamuhuri kufungua kesi ya jinai dhidi ya mfanyakazi aliyekwisha fukuzwa kazi kwa kosa husika au linaloendana kwa sehemu kuwa na kosa analoshitakiwa nalo.

Naamini lengo hapa ilikuwa na kulinda haki ya mfanyakazi na pia kuzuia maamuzi ya mwajiri kuingilia mwendeno wa kimahakama.

Siku nyingine unapoomba ushauri hasa wa kisheria kua waz na si kumeza maneno vinginevo utaambulia majib mafupi yenye tija ama yasio na tija kisha tatizo likabaki palepale la kutoelewa,
.
 
Kwa ufupi ni sahihi kutokana na maelezo yako mafupi, kufukuzwa kazi sio adhabu ya wizi pekee, kama sheria za kampuni zinasema kwa case za criminal mojawapo ya adhabu ni kufukuzwa kazi na kustakiwa basi kampuni ina haki ya kumshtaki

Tafadhali ushauri kama mwanasheria au kama siyo basi usiongee chochote. Kufukuzwa kazi ni hatua au adhabu ya kiutawala ila kosa la kughushi ni kosa la jinai ambalo huyo jamaa anapaswa ashtakiwe nalo na adhabu take ni kifungo cha miaka 7. Pia ni wa kushtaki kwa kosa longtime la uttering of a false document
 
Mi sijaona tofauti ya ulichoandika wewe na mimi, zaidi ya kubadirika kwa lugha tu
 
Back
Top Bottom